WATU sita wamekufa papo hapo na wengine 25 kujeruhiwa na kulazwa hospitalini kutokana na ajali mbili tofauti.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, alisema mjini hapa jana
kuwa ajali ya kwanza, ilihusisha basi la abiria lililokuwa na abiria 42,
ambalo liligonga kingo za daraja, likaparamia miti miwili kisha
kutumbukia ndani ya mto Lukosi, Iyovi eneo la Msosa huko Mikumi wilaya
ya Kilosa mkoani Morogoro, katika barabara kuu ya Iringa – Morogoro.
Alisema
tukio hilo ni la Januari Mosi mwaka huu majira ya saa 8 mchana. Basi
hilo lilitokea Dar es Salaam, lilikuwa linakwenda Mbeya.
Kamanda
Paulo alisema dereva wa basi hilo aliendesha gari kushoto zaidi,
akaenda kugonga kingo za daraja hilo, akaenda kuparamia miti miwili
kisha alilitumbukiza ndani ya mto huo.
Kamanda
huyo alisema katika ajali hiyo, watu watatu walikufa akiwemo dereva wa
basi hilo na kujeruhi wengine 16, ambapo majeruhi 14 walilazwa katika
Kituo cha Afya cha Tandika kilichopo eneo la wilaya ya Kilolo, mkoani
Iringa. Majeruhi wengine sita walisafirishwa hadi Hospitali ya Mkoa wa
Iringa na kulazwa.
Kamanda
alisema basi hilo lilibeba abiria 42 na chanzo za ajali hiyo kilielezwa
na mashuhuda kuwa ni uzembe wa dereva wa basi, aliyeshindwa kufuata
sheria za usalama barabarani katika eneo hilo la safu ya milima ya
Iyovi, lenye kona nyingi na mito yenye madaraja. Alisema maiti mmoja
ametambulika na ni dereva wa basi hilo.
Maiti
wawili, mmoja mwanamume na mwingine mwanamke, bado hawajatambuliwa na
wamehifadhiwa katika chumba za maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Morogoro. Alitoa mwito kwa watu kufika kuwatambua.
Kamanda
huyo wa Mkoa alisema ajali ya pili ilitokea Januari Mosi mwaka huu,
ambapo watu watatu walifariki papo hapo na wengine watano kujeruhiwa na
kulazwa katika Kituo cha Afya cha Gairo wilayani Gairo mkoani Morogoro.
Alisema
ajali hiyo ilihusisha gari ndogo, lenye namba za usajili T 252 CGV aina
ya Toyota Vitz, lililokuwa likiendeshwa na Bundala Charles Mahimbo,
mkazi wa Dar es Salaam. Gari hilo liligongana uso kwa uso na lori, lenye
namba za usajili T531 CFE lenye tela namba T 509 AFY aina ya Scania,
lililokuwa likiendeshwa na dereva, Ally Said Magimbi (33), mkazi wa
Mtongani , Dar es Salaam.
Alisema
ajali hiyo ilitokea jioni eneo la Ngiroli wilayani Gairo barabara kuu
ya Morogoro- Dodoma. Gari ndogo lilikuwa likitokea Mkoa wa Tanga kwenda
Mwanza wakati lori kubwa lilitokea Kagera kwenda Dar es Salaam.
Kamanda
Paulo alisema watu watatu waliokuwa katika gari ndogo, walikufa papo
hapo na wengine watano walijeruhiwa, miongoni mwao mmoja ni abiria wa
lori.
Kamanda
huyo wa Polisi aliwataja waliokufa katika ajali hiyo ni Bundala Mahimbo
ambaye ni mkazi wa Dar es Salaam, Flora Mugabo na Emmanuel Mahimbo,
wote wakazi wa Nyakato mkoani Mwanza.
Majeruhi
waliolazwa Kituo cha Afya Gairo ni dereva wa lori, Ally Magimbi, mkazi
wa Mtongani Dar es Salaam, Peter Mahinda ambaye ni mkazi wa Nyakato na
Hassan Mwera. Walioruhusiwa ni Judith Joseph na Scolastica Fransis
aliyekuwa abiria kwenye gari kubwa.
Kwa
mujibu wa Kamanda Paulo, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa
gari ndogo ambaye aliamua kulipita gari jingine kwenye kona na kwenda
kugongana uso kwa uso na lori hilo na kusababisha vifo vya watu hao na
majeruhi.
No comments:
Post a Comment
paulmkale