New Music : Meda Classic - Somebody | Download

Enjoy music from Meda Classic! The song titled "SOMEBODY"..

New Music: Harmonize - Kasuku | Download

Enjoy good music from Harmonize! The song titled "KASUKU" Download and Enjoy!!!!

New Video: Ostar Classic - Tutakupenda"Utanipenda Remix" (Official Video)

Enjoy video from Ostar Classic! this is song to reply diamond platnumz hit song titled "UTANIPENDA" and this version titled "TUTAKUPENDA".

New Video: Bill Nass ft TID - Ligi Ngogo (Official Music Video)


https://youtu.be/siRKpZcwinQ

Ratiba ya Ligi Kuu Uingereza wikiendi hii

Ligi Kuu Uingereza inatarajiwa kutimua vumbi wikiendi hii ambapo kutakuwa na michezo kadhaa ikiwemo Manchester United ikipambana na Stoke City katika dimba la Britannia.
Nao vinara wa Ligi Leicester City itakuwa Anfield ikipimana nguvu na Liverpool.
RATIBA KAMILI WIKIENDI HII

15:45 Stoke v. Man Utd

18:00 Aston Villa v. West Ham

18:00 Bournemouth v. Crystal Palace

18:00 Chelsea v. Watford

18:00 Liverpool v. Leicester

18:00 Man City v. Sunderland

18:00 Swansea v. West Brom

18:00 Tottenham v. Norwich

20:30 Newcastle v. Everton

22:45 Southampton v. Arsenal

Muda wote ni kwa saa za Afrika Mashariki.

New Video: Neyba - Uje (Official Video)

New Video: Mb Dogo - Sio Siri (Official Video)

Yanga imeizidi kete Simba katika utitiri wa mastraika 8...


YANGA imeizidi kete Simba katika utitiri wa washambuliaji baada ya usajili wa nyota wawili kwa mpigo; Paul Nonga na Issofou Boubacar ‘Garba’ ambao umeifanya kuwa na jumla ya washambuliaji nane, mmoja zaidi ya watani wao.
 

Wakati wadau wa soka wakijadili umuhimu wa Nonga katika jeshi lililosheheni washambuliaji wakali, Yanga wamekuja juu na kusema kuwa na ingewezekana wangeendelea kuongeza wengine kwani wanataka kuwa na kikosi kipana zaidi.
 

Safu ya mbele inaundwa na; Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Garba, Nonga, Matheo Simon na Malim Busungu, wakati huohuo kuna viungo washambuliaji Geoffrey Mwashuiya na  Simon Msuva ambao pia wanao uwezo wa kufunga.
 

Akifafanua kiufundi zaidi, Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, ameliambia Championi Ijumaa kuwa, benchi lilifikia uamuzi huo kutokana na wingi wa mashindano yanayowakabili, ikiwemo Ligi ya Mabingwa Afrika (Caf).
 

“Ukiangalia tuna michuano mingi ambayo inatulazimu kuwa na kikosi kipana zaidi. Caf, ligi kuu, Kombe la FA na hapohapo Mapinduzi inatusubiri siku chache zijazo.
“Hivyo kuna kila sababu ya kuwa na kikosi kipana, siyo kuwategemea wachezaji walewale (Donald) Ngoma na (Amissi) Tambwe, wakiumia je?
“Hivyo lazima uwe na kikosi kipana ili kama ni kasi ya kushambulia kusionekane pengo michuano kwa michuano,” alisema Mwambusi.

Yanga Vs Mbeya City Kikosi cha kwanza Yanga hiki hapa

YANGA imeendelea kuonyesha kuwa haitaki utani katika msimu huu wa 2015/16, hiyo ni kutokana na mazoezi ambayo timu hiyo imekuwa ikiyafanya lakini zaidi ni kuwa kikosi cha kwanza kipo kamili.

Yanga itakutana na Mbeya City, kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara lakini tayari Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, ameshapata kikosi kitakachocheza mchezo huo na mbadala wa wale ambao watapata matatizo au kuwa nje ya uwanja kwa sababu yoyote ile.

Katika mazoezi ya jana asubuhi kwenye Uwanja wa Boko, Beach Veteran nje kidogo ya Dar, kocha huyo alipanga vikosi viwili na kucheza kama mechi kati ya hivyo vyote kilikuwepo kimoja alichoonekana akikiandaa zaidi kwa kukipa mbinu nyingi.

Kikosi kinachoaminika kuwa ni cha kwanza na kitaanza katika mchezo wa kesho kiliundwa na; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Vincent Bossou, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Deus Kaseke, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Simon Msuva.

Kikosi cha pili ambacho ni wazi kinaweza kuwa mbadala wa nafasi za wale waliopo kwenye kikosi cha kwanza kiliundwa na; Benedicto Tinoko, Oscar Joshua, Salum Telela, Pato Ngonyani, Hassani Mwakipa, Juma Makapu, Geofrey Mwashiuya, Malimi Busungu, Paul Nonga, Matheo Anthony na Boubacar Garba.

Ikiwa kikosi cha kwanza kitapangwa hivyo maana yake ni kuwa, Msuva na Kaseke ambao walikuwa wakipata nafasi katika kikosi cha kwanza kimachale, watakuwa wamechukua nafasi ya Busungu aliyekuwa akipangwa kushambulia akitokea pembeni.

Upande wa wachezaji wapya waliotua hivi karibuni, Nonga na Boubacar bado wanahitaji muda ili kocha awaone na kuna uwezekano wakaingia wakitokea benchi katika mchezo huo.

Katika mazoezi hayo, Pluijm alikuwa akiwataka wachezaji wake kucheza soka la pasi za haraka, huku Ngoma na Kamusoko wakionekana kivutio kutokana na aina ya soka lao kuwafurahisha waliojitokeza uwanjani hapo.

Kuhusu mchezo huo wa kesho, Pluijm alisema: “Maandalizi ya kikosi changu yanaendelea vizuri na tunachosubiri ni ushindi tu.

“Katika mazoezi ya leo kama ulivyoona, nilikuwa nikisisitiza wachezaji wangu kucheza soka la pasi za haraka wakati tukiwa na mpira tunashambulia goli la wapinzani, hiyo yote ni katika kuhakikisha tunapata matokeo mazuri.”

New Music: Neyba - Uje | Download


Download and Enjoy New Music from NEYBA, the song titled "UJE".

Mbunge ampa Wema Sepetu Ujauzito...Wema furaha tupu!


MJINI bwana! Habari nyingi huanzia kwenye mikeka, siku hizi wenyewe wamezimebatiza jina la ‘Ubuyu’ ambapo kwa sasa ishu kubwa inayozagaa mitaani ni mwigizaji Wema Sepetu ‘Madam’ kupachikwa mimba na mbunge maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Bunge la 11 (jina kapuni kwa sasa), vyanzo vinasema.

Pitapita ya sikio la Gazeti la Ijumaa katika Jiji la Dar es Salaam, hivi karibuni ilikutana na Ubuyu huo kuwa mwigizaji huyo amenasa ujauzito wa mwanasiasa huyo ambaye ni kijana mwenye utajiri mkubwa anayetajwa kwa sasa kumiliki vilivyo penzi la Madam.


KUMBUKUMBU KABLA YA HABARI
Kwa muda mrefu, Wema amekuwa akihaha kusaka mtoto baada ya kupitia kwenye uhusiano na wanaume tofauti akiwemo Yusuph Jumbe, Steven Kanumba (marehemu), Nasibu Abdul ‘Diamond’ na CK (yule kigogo).

Akiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaume hao kwa hesabu yake na nyakati tofauti, mara kadhaa msanii huyo maarufu amekuwa akikebehemiwa na mahasimu wake kuwa ni mgumba jambo ambalo limekuwa likimhuzunisha.

HABARI KAMILI
Ijumaa baada ya kuzinasa habari za ujauzito wa msanii huyo, lilijongea kwenye vyanzo vyake na kukutana na ushuhuda huu kutoka kwa rafiki wa karibu wa Wema ukisema: “Suala la mimba sijui lakini Wema na mheshimiwa wana uhusiano.
“Ukaribu wao ulianza wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu (Wema alikuwa akimnadi mgombea urais wa CCM, John Magufuli), mpaka leo wanaendelea.”

MIMBA KABAAH!
Baada ya chanzo cha karibu na Wema kutoboa mfereji wa uhusiano na kuliacha suala la ujauzito kwenye sintofahamu, wachapakazi wa Ijumaa waligeuza masikio yao upande wa mheshimiwa mbunge ili kupata ubuyu mwingine ambapo suala la mimba lilitajwa waziwazi.

“Sitaki kunukuliwa ila mimi nimemsikia mheshimiwa akidokeza kuwa Wema ni mjamzito, kwangu mimi kama rafiki yake naona ni jambo jema, hiyo ndiyo kazi ya mwanaume kaka...hahahahaha!” Mmoja kati ya marafiki wa mbunge huyo alisema na kumalizia kwa kicheko.

WEMA NA MBUNGE FULL KICHEKO
Inaelezwa na vyanzo vyetu kuwa baada Wema na mbunge huyo kuwa wazazi watarajiwa wote kwa pamoja wamekuwa na furaha ya aina yake huku kila mmoja akimsisitiza mwenzake kuwa makini ili upepo mbaya usipite kati yao.

Aidha, katika hali inayoashiria kuwepo kwa kitu cha tofauti kwa msanii huyo aliyepata kuwa Miss Tanzania 2006, hivi karibuni aliandika kwenye akaunti ya Instagram kuwa anayo sapraizi ya nguvu kwa mashabiki wake.

Baadhi ya wadau wa masuala ya burudani wamehusisha sapraizi aliyoitangaza Wema na habari za ujauzito wake unaotarajiwa kumaliza kejeli juu yake kuwa yeye ni sawa na mti usiozaa kwamba hauna thamani.

MBUNGE NI TAJIRI MKUBWA
Mbali na umaarufu wa mbunge huyo timu ya Ijumaa ilijiridhisha kuwa mwanasiasa huyo ni tajiri anayemiliki migodi ya madini na kufanya biashara mbalimbali zikiwemo za usafirishaji mizigo na abiria anazofanya kupitia magari yake.

Kutokana na utajiri huo, habari zinadai kuwa mbunge huyo ndiye anayempa jeuri ya fedha Wema ambayo inamfanya aishi maisha ya ‘nyodo’ kama wasemavyo watoto wa mjini.

WEMA, MBUNGE WATAFUTWA
Katika kukamilisha weledi wa habari, gazeti hili lilimtafuta mbunge huyo kwa njia ya simu ili azungumzie ishu hiyo lakini hakuweza kupatikana hewani jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa jina lake kuhifadhiwa.

Kwa upande wa Wema naye hakuweza kupatikana kwa namba zake za simu sambamba na ile ambayo chanzo chetu kilisema ni mpya jambo linaloifanya habari hii kuwa na mwendelezo baada ya kujiridhisha kwa kupata kauli za pande zote mbili.

AUNT ANENA
Kama haitoshi gazeti hili lilimtafuta shosti wake wa karibu na Wema, Aunt Ezekiel ili naye afunguke kidogo juu ya madai ya ujazito wa rafiki yake ambapo mahojiano yalikuwa hivi:

Ijumaa: Mambo anti’ake?
Aunt: Safi cha umbea wangu, nipe mpya.
Ijumaa: Naona shosti yako Wema karudi ili umpe mafunzo ya kulea mimba, mpe hongera zake, kushika mimba ya mbunge si jambo dogo.

Aunt: Kwani kakuambia yeye mwenyewe? Kwanza niko naye hapa, anasema simu zako amekuwa anaziona lakini hataki kupokea.
Baada ya mazungumzo hayo ilisikika sauti ya Wema ikisema: “Tena mwambie ni ya miezi 6, tatizo nini?”
CHANZO: GAZETI LA IJUMAA

Mwambusi avujisha siri za Mbeya City



Dar es Salaam
KOCHA wa Yanga, Hans van Der Pluijm, kwa siku mbili mfululizo alionekana kuvalia njuga programu ya soka la kutibua na soka la nguvu huku mashambulizi yakipitia wingi zote.
Kikosi hicho kinaendelea na mazoezi yake kwenye Uwanja wa Boko Veterani, kujiweka tayari kumenyana na Wagonga Nyundo wa Mbeya City, timu ya zamani ya Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi.
 

Si kawaida ya Pluijm kukomaa na programu ya ‘fiziki’ na alipoulizwa, alikiri kufanya vile kutokana na aina ya soka la wapinzani wao kuwa la ‘minguvu’ tu.
Mdachi huyo aliongeza kuwa tayari amejua jinsi ya kuwamaliza kwani anajivunia uwepo wa Mwambusi ambaye anaijua fika Mbeya City, hivyo kwa kiasi kikubwa ni msaada wa kuwakabili pasipo shaka.
 

“Kweli nilitaka kujaribu mfumo wa soka la nguvu kutokana na upinzani wenyewe. Nimekutana nao kama mara tatu, lakini mfumo wao ni uleule (nguvu), hivyo tumeona kuna kila sababu ya kulifanyia kazi.
“Itakuwa mechi ngumu kutokana na mfumo wao, lakini kwa upande mwingine najivunia kuwa nina mtu ambaye anawafahamu vizuri (Mwambusi) nafikiri haitakuwa shida sana,” alifunguka Mdachi huyo kwa furaha.

Shoo ya kifalme... Diamond ndani ya DAR LIVE leo

MWANDISHI WETU
Dar es Salaam
SIKUKUU ya Krismasi si ndiyo leo? Jibu ni ‘ndiyooooo!’, sasa habari kamili ni kuwa wakazi wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani, wote wanatarajiwa kukutana kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem ambapo Simba wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ atakuwa akifanya makamuzi.
Diamond, staa ambaye anasadikika kupata umaarufu mkubwa nje ya mipaka ya nchi zaidi ya wasanii wengi wa Bongo Fleva katika historia ya muziki huo, atakuwa akitambulisha kwa mara ya kwanza wimbo wake wa Utanipenda?
Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo amefunguka kuwa burudani itaanza rasmi asubuhi maalum kwa watoto ambapo kutakuwa na michezo mingi ikiwemo kuteleza, kubembea, kupanda ndege maalum, kuogelea kwenye bwawa kubwa la kisasa na mingine mingi.
“Watoto wote wanaruhusiwa kuja kwa kiingilio kidogo cha shilingi 2,000 tu na kupata burudani zote hizo hadi saa kumi na mbili jioni kisha itafunguliwa rasmi shoo ya wakubwa,” anasema Mbizo.

Diamond:
Nitakamua shoo live
Kuelekea shoo yake ya leo pale Dar Live, Diamond anasema: “Kwanza nitatoa zawadi kwa mashabiki wote watakaotoka bomba siku ya shoo ikiwa ni pamoja na kupiga nao picha na kuzungumza nao mawili matatu kabla sijapanda jukwaani.
“Pia nitafanya shoo ya ‘live’, ambapo nitakuwa pamoja na timu yangu nzima ya Wasafi Classic Baby (WCB). Ngoma zangu zote kali nitaziimba zikiwemo Mbagala, Mdogomdogo, Nasema Nawe, Nana, Nitarejea, Nataka Kulewa, Kesho, Moyo Wangu na huu ambao ni wimbo wa taifa kwa sasa, Utanipenda?”

Msagasumu, Diamond uso kwa uso
Bingwa wa muziki wa Singeli, Msagasumu naye atakuwepo jukwaani kupiga shoo kali.
Unajua amesemaje jamaa? Ah ah ah ah ana mbwembwe balaa, msikie hapa. “Siku zote nikiwa Dar Live huwa sikosei, nitapiga ngoma zote kuanzia Shemeji Unanitega, Huyu Mtoto, Inaniuma Sana na Naipenda Simba, yaani kwa ufupi nitafunikaaa!”
Wakali Dancers kudansi 100%
Kuthibitisha kuwa Sikukuu ya Krismasi inakwenda vizuri, mashabiki pia wategemee kuliona kundi linalobamba Afrika Mashariki upande wa kudansi, Wakali Dancers nao watakuwa jukwaani kufanya kweli.

Mshindi Ijumaa Sexiest Girl huyu hapa
Wafuatiliaji wa shindano la mwanamke mwenye mvuto (Ijumaa Sexiest Girl 2015) linaloendeshwa na Gazeti la Ijumaa kwa mara nyingine watapata fursa ya kuwashuhudia live washiriki wote walioshiriki shindano hili sambamba na kutangazwa mshindi.
Shindano hili ambalo limedhaminiwa na Hamadombe Distributor limebakiwa na washiriki watatu walioingia fainali ambao ni Asha Salum ‘Kidoa’, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Vanessa Mdee ‘Vee Money’, leo usiku mshindi atajulikana.
Miongoni mwa zawadi atakazoibuka nazo mshindi wa shindano hili ni fedha taslim, tuzo, cheti, ofa ya bure ya kufanya shopping ya nguo na kutengenezwa nywele kwa kipindi cha miezi sita.

Unaingiaje Dar Live? Soma hapa
Burudani yote hiyo itakuwa ni kwa kiingilio cha shilingi 15,000 (kawaida) huku V.I.P ikiwa ni shilingi 30,000 tu.
Mbali na kiwango hicho, wadhamini wakuu wa shoo hii ambao ni Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi Airtel, kupitia huduma yao ya kijanja kimawasiliano ya Airtel Money Tap Tap watatoa punguzo la kiingilio kwa tiketi 1,000 za awali endapo utakata kwa kutumia huduma hiyo mpya.
Unachopaswa ni kuwa na kadi yako ya Airtel Money Tap Tap ambayo inapatikana kwa mawakala wote wa Airtel waliopo Temeke na Ilala na ukifika nayo Dar Live utapata punguzo la Sh 5,000 yaani tiketi ya Sh 15,000 utapata kwa Sh 10,000 na ya Sh 30,000 itakuwa Sh 25,000.


New Video: Prezzo - Mrembo (Official Video)

New Video: Eric Omondi - Royal (Official Video)

Comedian Eric Omond drop his new video titled "ROYAL" Download and Enjoy!!!

New Video: Eric Omondi - Je Utanipea (Official Video)

New Music: Izzo Bizness Ft.Navio & Mwasiti-Walala Hoi ( Part2 ) | Download

Ben Pol ampigia magoti Alikiba, wayamaliza, huenda wakafanya collabo

Jana December 23 2015 gossic cop wa show ya XXL #CloudsFM, Soudy Brown alifanikiwa kumpata Alikiba… maswali ya Soudy kwa Alikiba ilikuwa jinsi alivyopokea maneno ya Ben Pol kwenye post ya Twitter ambayo alimtaja !!
Alikiba alisema hana neno na wala hana tatizo na Ben Pol, kwa hiyo hata kilichoandikwa na Ben Pol alikichukulia poa kabisa… leo Alikiba alikuwa ‘live’ kwenye show ya Jahazi Clouds FM, baada ya stori mbili tatu watangazaji Emmanuel Likuda na ‘Mtembezi’ Antonio Nugaz wakaona wamcheki pia Ben Pol ili kujua sababu ya kuweka post ya kumhusu Alikiba na muziki wake.Unajua Alikiba ni kama kaka, alivyolichukulia hili suala najua kalichukulia kama kaka… suala la msingi, Watanzania wajue kwamba tuko sawa na Kiba… tukiwa tunazunguka haitakuwa kitu kizuri… tutakiane heri kwa sababu tumekuwa na mwaka mzuri.’- Ben Pol.
Kwenye sentensi nyingine Ben Pol ameendelea hivi >>> ‘Haijalishi nani kajishusha kuomba radhi lakini suala la msingi ni kwamba mimi na Kiba tuko sawa…
Alikiba nae akaongea haya wakati Ben Pol akiwa hewani bado >>> ‘Nimekusamehe lakini nilishtushwa kama watu wengine walivyoshtuka… ni binadamu tunakuwa na makosa wakati mwingine…
Ben Pol nae akamalizia >>> ‘Huwezi jua mipango ya MUNGU, hatujui hapo mbeleni inaweza kutokea bonge la collabo yetu

New Video:Criss Wamarya - Cheusi Mangala (Official Video)

This song Cheusi mangala Has Been Produced By Mazuu from Tanzania and Writen by Criss Wamarya.The Video was Stoot in Morogoro Tanzania by GQ

New Video: Iyanya - Christmas Special (Official Video)

Mwimbaji kutoka Nigeria Iyanya amewapa mashabiki wake zawadi kubwa kwaajili ya X Maxx, hii video yake mpya ya  ‘O Come All Ye Faithful‘ itazame hapa.


Kaa tayari kuipokea zawadi siku ya ‘boxing day’ kutoka kwa Alikiba December 26 Dar es Salaam..

Star wa muziki Bongo, Alikiba a.k.a ‘King Kiba‘ ambaye siku chache zilizopita ameachia ngoma yake na mkali wa masauti, Christian Bella amekuja na good news ambayo ni zawadi tutakayoipokea December 26 2015 siku ya boxing day !!Tumeona post nyingi za Alikiba akiwa kwenye show nje ya TZ, ikiwemo Ulaya na Marekani, Alikiba kaona zawadi yake ya Christmas atashare na Wana-Dar es Salaam wa nguvu.. zawadi yenyewe ni show ya nguvu pale Escape 1, mzigo wake utakuwa nonstop kwenye stage yeye pamoja na bendi yake.

New Music: Jamali Selemba X Sharoom ft Harmonize - Uzuri Tabia | Download

Diamond Platinumz akacha shoo ya zari.


Habari ya mjini! Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amezua utata kwa mashabiki wake baada ya kukacha kuzama kwenye pati iliyokuwa imeandaliwa na mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Guvnor jijini Kampala, Uganda ambapo wawili hao walikwenda pamoja kwa lengo la kushirikiana kwenye makamuzi ya shoo ya pati hiyo iliyokwenda kwa jina la Zari All White Ciroc Party.
 Zari All White Ciroc Party
Ilielezwa kwamba, tofauti na matarajio ya wengi, Diamond hakuonekana ukumbini badala yake aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Ssemwanga akawa anajitanua ukumbini humo akiwa na rafiki zake huku Pedeshee Jack Pemba wa Bongo akigandana na Zari muda mwingi.
Baada ya kumwagiwa ‘ubuyu’, Ijumaa Wikienda kama kawaida yake lilimtafuta Diamond kwa lengo la kutaka kujua kilichomkwamisha kwenda kwenye makamuzi ya mzazi mwenzake huyo ambapo alisema alishindwa kuhudhuria baada ya promota wake kumzuia kwenda ‘kumkampani’ Zari akihofia kuzorotesha makamuzi yake yaliyopangwa kufanyika siku iliyofuata kwenye Viwanja vya Lugogo Cricket Oval jijini Kampala.
 ZARI834
“Nilikuwa na hamu mno ya kumpa kampani mama Tiffah lakini nilizuiwa na promota wangu kuhofia kama ningeonekana ukumbini basi ningeweza kumvurugia shoo yake maana aliniambia nisionekane kabisa, nadhani tageti yake ilikuwa ni kuhakikisha watu wananishuhudia siku ya shoo yangu tu,” alisema Diamond.
Kufuatia kukosekana kwa Diamond kwenye pati hiyo, watu walijikuta wakinong’ona ukumbini wakitaka kumuona kwani walishajua kuwa yupo jijini Kampala.

Aunty Ezekiel : Mdogo wa Cookie anakuja soon!!




STAA maarufu wa fi lamu Bongo, Aunty Ezekiel amefungua kinywa chake na kusema STAA maarufu wa fi lamu Bongo, Aunty Ezekiel  kuwa kwa sasa yuko kwenye mchakato wa kumtafuta mdogo wake na Cookie kwa kuwa hataki kukaa muda mrefu ili kwa kuwa hataki kukaa muda kupata mtoto mwingine.
 
Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni  Aunty,alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kwa ameamua kufanya hivyo kwa kuwa anaona kuzaa mapema na kumaliza ndiyo poa ili aweze kuendelea na kazi zake vizuri kuliko kukaa muda mrefu halafu ndiyo ubebe ujauzito
tena. “Sasa hivi mimi na baba Cookie tumeshaamua kufanya maamuzi mazuri kabisa ya kuongeza mtoto mwingine maana tumeona kwanza ndiyo furaha yetu

Wema sepetu Atimuliwa kenye nyumba kisa Skendo ya maji na Umeme!

UFALME umeanguka! Unaweza kusema hivyo! Hatimaye Miss Tanzania 2006, aliye pia staa wa filamu za Bongo, Wema Isaac Sepetu amedaiwa kutimuliwa kwenye nyumba ambayo alipanga kwa mbwembwe na kualika waandishi wa habari ili watoe ‘nyuzi’ hewani, akidai ni yake kwa kuinunua kwa shilingi milioni 280, fuatana na Ijumaa Wikienda. Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Wema amekumbwa na kadhia hiyo ya kuhamishwa kwenye nyumba hiyo iliyopo Makumbusho jijini Dar, usiku wa Desemba 18, mwaka huu. 
 
SIKIA CHANZO
 “Jamani mmesikia kilichomtokea Wema Sepetu? Yaani huyu dada anaishi kwa maigizo hadi basi. Lile sakata lake la kudaiwa kutumia umeme na maji kimagumashi limemtokea puani, maana kwenye umeme pekee yake nasikia anadaiwa zaidi ya shilingi milioni nane (8,000,000) fedha ambazo imekuwa shida kulipa.”
 BABA MWENYE NYUMBA
AINGIA KATI “Sasa baba mwenye nyumba ameingilia kati. Ameamua kulipa yeye deni hilo lakini akamtaka Wema ahame haraka  kwenye nyumba yake,” kilisema chanzo.

 SIKU YA TUKIO Paparazi wetu alizidi kupenyezewa ‘ubuyu’ kuwa, muda huo tayari kuna lori aina ya Toyota Canter linahamisha vitu nyumbani kwa Wema na kwamba, kuna kila dalili anahama baada
ya baba mwenye nyumba wake kumtimua.




 PAPARAZI NYUMBANI KWA WEMA
Ilibidi paparazi wetu akimbie kwa pikipiki iendayo kasi mpaka nyumbani hapo na kukuta kweli lori likibeba vitu mbalimbali huku wabebaji wakitokwa jasho chapachapa. Gari hilo lilisimama kwenye lango kuu la kuingilia ndani ya nyumba hiyo huku likiwa na shehena ya mafurushi ya mizigo. Wakati paparazi wetu akiwa kwenye hali ya mshangao, aliendelea kuona mizigo mbalimbali ikitoka ndani ya mjengo huo huku vyombo anuai vya ndani, kama kabati na baadhi ya makochi yakiwa nje ya nyumba hiyo yakisubiri kupakiwa tayari kwa  safari ya kumuondoa Wema kwenye mjengo huo. 


WEMA HAYUPO 
Swali la kwanza kwa wabebaji hao kutoka kwa paparazi wetu ni wapi alipo Wema. “Unamtaka Wema wa nini wakati
unajua hayupo hapa, kwanza wewe nani?” alikuja juu mpakiaji mmoja.

PAPARAZI ANUSURIKA KIPIGO
Katika hatua nyingine isiyokuwa ya kawaida, wapakiaji wengine walitaka kumshushia kipigo paparazi wetu baada ya kuona mwanga wa kamera wakati akichukua picha kadhaa kwa ajili ya ushahidi. WALIKOHAMIA Uchunguzi wa awali, Wema amehamia Mbezi Beach, Dar. Hata hivyo, tangu sakata la wizi wa maji na umeme, Wema hajawahi kulala na kuamka ndani ya nyumba  hiyo huku habari zikisema amekuwa akiishi mahotelini kama ‘digidigi’. 


KWA NINI WEMA ALISEMA NYUMBA  NI YAKE? “Kuna watu wengi walikuwa hawatambui kwa nini Wema awali alisema hii nyumba ni yake. Mwanzo wakati anahamia, pia alikuwa ana mazungumzo na baba mwenye nyumba kwamba ainunue lakini watoto wakagoma hivyo Wema akawa analipa kodi kila mwaka.

WEMA, PETIT MAN Juzi, Wema hakupatikana hewani ili kujibu madai hayo, lakini mmoja wa watu wake wa karibu, Petit Man alikumbana na paparazi wetu katika klabu moja jijini Dar, alipoulizwa kuhusu mambo hayo alikiri Wema kuhama kwenye nyumba hiyo. “Tena sasa tunahamia kwenye nyumba aliyonunua Wema mwenyewe. Bonge la nyumba, mtaipata habari yake. Iko Mbezi Beachn alisema Petit.

Mbowe: John Pombe Magufuli Anacheza Ngoma ya Chadema...Adai CCM Imemdhibiti Katika Uteuzi wa Baraza la Mawaziri

 
Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema anafurahi kuona Rais John Magufuli akitekeleza sehemu kubwa ya sera za chama chake na kwamba kazi ya upinzani si kupinga kila kitu, bali kuangalia masilahi mapana ya Taifa.

Mwenyekiti huyo pia amesema “biashara imeisha” kwa Rais John Magufuli baada ya kutoka kwenye kikao cha Kamati Kuu ya CCM kwa kuwa chama hicho kilimdhibiti katika uteuzi wa Baraza la Mawaziri kiasi cha kumfanya arudishe sura zilezile.

Rais ameanza kazi kwa kishindo baada ya kufumua uozo kwenye taasisi mbalimbali za Serikali kama Mamlaka ya Bandari (TPA), Mamlaka ya Mapato (TRA), Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), huku akidhibiti matumizi ya Serikali kwa kubana safari za nje za watumishi wa umma, kuondoa posho za vikao na pia kuanza utekelezaji wa ahadi ya elimu bure.

Mbowe anaona mambo hayo ndiyo ambayo wapinzani wamekuwa wakipigia kelele wakati wote.

Akizungumza kwenye kipindi maalumu cha Kituo cha Televisheni cha Azam juzi, Mbowe alisema hakuna jambo ambalo Rais Magufuli analifanya ambalo kambi ya upinzani haijawahi kulizungumzia.

Alitaja baadhi ya mambo hayo kuwa ni hoja ya kubana matumizi ya Serikali, kupunguza safari za nje za viongozi na kupunguza idadi ya watumishi wasio wa lazima.

Mambo mengine alisema ni kupunguza sherehe za kitaifa na kuwa na Serikali ndogo. Alisema kwa kiasi kikubwa Rais anatekeleza sera za upinzani ambazo zilikuwa zinapingwa na wabunge wa CCM.

“Kuwa mpinzani haimaanishi kupinga kila jambo linalofanywa na Serikali hata kama jambo lenyewe ni jema. Ni wajibu wetu kama upinzani kuisimamia Serikali ili kuhakikisha kwamba kila analolisema Rais linatekelezwa kwa vitendo,” alisema Mbowe ambaye pia aligombea urais bila mafanikio mwaka 2005.

Mbunge huyo wa Hai aliongeza kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani itaendelea kutimiza wajibu wake wa kusimamia mambo yenye masilahi kwa wananchi na haitaona haya kuikosoa Serikali pale inapotoka kwenye mstari.

Dk Magufuli ameanza urais kwa kufuta safari za nje hadi kwa kibali cha Ikulu, kumuondoa kaimu mkurugenzi mtendaji wa MNH na kuvunja bodi ya hospitali hiyo, kumuondoa kamishna mkuu wa TRA, mkurugenzi mkuu wa Takukuru, mkurugenzi mkuu wa TPA na katibu mkuu wa Wizara ya Uchukuzi kutokana na udhaifu alioukuta kwenye taasisi zao. Pia, ameanza kutekeleza ahadi ya elimu bure kwa kuagiza walimu wakuu kutolipisha wanafunzi ada kuanzia Januari na kufuta michango ya aina yoyote shuleni.

Pia, ametangaza Baraza la Mawaziri lenye watu 34, kufuta sherehe za maadhimisho ya Uhuru, Siku ya Ukimwi na kupongeza wabunge, akielekeza fedha zilizopangwa kwa shughuli hizo kuelekezwa katika kutatua matatizo ya wananchi.

Mbowe pia hakusita kukosoa Baraza la Mawaziri lililotangazwa na Dk Magufuli.

“Hakuna kipya,” alisema Mbowe.

“Sura ni zilezile zilizokuwapo kwenye Serikali iliyopita na baadhi ya mawaziri wanakabiliwa na kashfa.”

Mwenyekiti huyo alitoa mfano mfano wa uteuzi wa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe kwamba haukuwa sahihi kwa sababu ndiye aliyeteua bodi ya Bandari ambayo imevunjwa na Rais kutokana na usimamizi mbovu.

Aliongeza kuwa kurudi kwa Profesa Sospeter Muhongo pia si sahihi kwa sababu aliondolewa kwa uamuzi wa Bunge kutokana na kashfa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow.

Alisema Baraza la Mawaziri halina jipya kwa sababu Rais Magufuli alidhibitiwa na Kamati Kuu ya CCM katika kuliunda.

“Rais alifungwa mikono na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi na tangu ametoka Kamati Kuu biashara imeisha,” alisema Mbowe.

Lakini Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alimjibu Mbowe kuwa walitegemea kauli kama huyo kutoka kwa mwenyekiti huyo wa Chadema.

“Mwenyekiti wa Chadema angesifia uteuzi wa Baraza la Mawaziri, ningeshangaa sana,” alisema Nape, ambaye ni pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.

“Alichokisema ndicho wengi tulichokitarajia. Maoni ya Mbowe ni ushahidi wa jinsi asivyojua hata Katiba ya nchi inayoeleza mamlaka ya Rais juu ya uteuzi wa Baraza la Mawaziri kuwa haingiliwi na yeyote.

“Namshauri arudi shule kwa kuwa itamsaidia kuelewa kidogo.”

Picha: Diamond Platnumz Akiwa na Watoto Wote wa Zari

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii mwanadada Zarinah Hassan ‘Zari the boss Lady’ ambaye ni mzazi mwenza wa mkali wa bongo fleva, Diamond Platinum alitupia picha hizi akiwa yeye, Tiffah na Diamond pamoja na watoto watatu wa zari ambao diaomond alimkutanao kuandika maeno kuashiria hiyo ndiyo familia.

Hii ni kwama mara ya kwanza kwa diamond kupiga picha na watoto hao wa zari tangu Diamond awe na mahusiano na mwanadada Zari.

Jionee picha hizo hapo chini

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Jipatie tiketi ya bure shoo ya Diamond Krismasi

UNATAKA kwenda shoo ya Diamond, Krismasi hii? Kama ndiyo, sasa unaweza kujipatia tiketi ya bure kwenda kwenye shoo hiyo kwa kujibu maswali katika Gazeti la Uwazi kesho Jumanne pamoja na Risasi Mchanganyiko siku ya Jumatano.
Jinsi ya kushiriki, nunua gazeti lako la Uwazi au Risasi Mchanganyiko kisha jibu maswali kiufasaha ndani ya magazeti hayo katika kuponi maalum na washindi watano kila gazeti watajishindia tiketi ya bure kwenda kwenye shoo ya Diamond itakayofanyika Krismasi katika Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Wanaoruhusiwa kushiriki ni wenye umri kuanzia miaka 18, shindano hili ni kwa watu waishio jijini Dar pekee.

New Video: Eddy Kenzo - Soraye (Official Video)

Hii video mpya ya Eddy Kenzo ‘Soraye’ itazame hapa.


New Video: Witnesz Kibonge Mwepec - Buku Jero (Official Video)

New Music: Best Nasso - Rumba | Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/54857

New Video: Best Nasso - Rumba (Official Video)


New Video: Alikiba & Christian Bella – Nagharamia (Official Video)

Video iliyosubiriwa kwa hamu kubwa sana na mashamiki miongoni mwake ni hii ya mkali Alikiba akimshirikisha Christian Bella. Wimbo unaitwa Nagharamia sasa unaweza kuplay na kuitizama hapa kisha tume maoni yako na pongezi kwake.

New Video: Ommy Dimpoz - Achia Body (Official Video)