Tangaza hapa 'Advertise your Business here Page view per day 300,000 - 650,000'

Rais Magufuli Amuongezea Mwaka Mmoja Mkuu wa Majeshi Jenerali David Mwamunyange...Afanya Uteuzi wa Makamanda Wengine wa JWTZ


RAIS John Magufuli amemwongeza muda wa mwaka mmoja Mkuu wa  majeshi ya ulinzi nchini,Jenerali David Mwamunyange, ambaye alitakiwa kustaafu leo baada ya kutimiza umri  kwa mujibu wa katiba na sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mapema kwenye Makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyopo  Upanga jijini Dar es salaam,Jenerali Mwamunyange amesema leo alitakiwa kuungana na Brigedia wanne wa Jeshi la ulinzi nchini  pamoja na Meneja Jenerali  wawili  ambapo wote kwa  pamoja wamestaafu ndani ya Jeshi kwa mujibu wa sheria ya jeshi hilo.

“Mimi mwenyewe ilikuwa nistaafu kazi leo tarehe 30 Januari 2016,lakini Rais na Amri Jeshi mkuu ameamua kunibakiza katika utumishi jeshini kwa mwaka mmoja kuazia leo tarehe 30 januari,2016 hadi tarehe  31 Januari 2017,” amesema Jenerali Mwamunyange

Jeneral Mwamunyage amesema sababu iliyomfanya Rais Magufuli kumwongezea mda huo imetokana na Rais kutopata mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo aliyonayo .
 
Hata hivyo, Jenerali Mwamunyange amesema Rais Magufuli amemteua  Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa mnadhimu mkuu wa Jeshi la ulinzi la wananchi.

Sanajari na huyo,Jeneral Mwanunyange amesema pia Rais Magufuli  amefanya uteuzi mkubwa ndani ya Jeshi hilo  kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya jeshi hilo.
 
Jenerali Mwamunyange ametaja walioteuliwa na Rais  ni Meja Jenerali James Aliois Mwakibolwa  kuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la nchi Kavu ambaye amechukua nafasi ya meja Jenerali Salum Mustafa Kijuu anayestaaafu kazi leo baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria ambapo Meja Mwakibolwa alikuwa ni mkuu wa tawi la utendaji wa kivita na mafunzo makao mkuu ya jeshi.

Jeneral Mwamunyange alimtaja pia  kamanda mwingine aliyeteuliwa na Rais ni Meja Jenerali Yakub Sirakwi kuwa  Mkuu wa chuo cha ulinzi wa Taifa (Commandant NDC) kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Gaudence Milanzi ambaye ameteuliwa na Rais kuwa Katibu mkuu wa wizara ya Maliasilia na utalii. Meja Jenerali Sirakwi alikuwa mratibu msaidizi mkuu baraza la usalama wa Taifa- BUT.

Mwingine  aliyeteuliwa  na Rais Magufuli ni Brigedia Jenerali George William Ingram kuwa  Mkuu wa Kamandi ya jeshi la Anga ambaye anachukua nafasi ya  Meja Jenerali Joseph  Pwani aliyestaafu leo kisheria  baada ya kufikisha umri wa kustaafu. Bregedua Jenerali Ingram alikuwa Afisa Mnadhimu katika mako makuu ya kamandi ya Jeshi la Anga.

Pia Rais Magufuli amemteua Bregedia Jeneralio M.W Isamuhyo  kuwa  Mkuu wa jeshi la Kujenga Taifa,kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Raphael Muhuga anayestaafu kazi leo,baada ya kufikisha umri wa kustaafu kazi kisheria,kabla ya uteuzi Bregedia Isamuhyo alikuwa mkurugenzi makao mkuu ya jeshi.

Vilevile Rais Magufuli amemteua Bregedia Jenerali Jacob Kingu  kuwa   mkuu wa shirika la mizinga  kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Charles Muzanila anayestaafu leo kisheria baada ya kufikisha umri .Brigedia Jeneral Kingu alikuwa mkuu wa utawala na mafunzo katika makao mkuu ya jeshi la kujenga Taifa.

Pia Rais Magufuli  amemteua Bregedia Jenerali Robison Mwanjela kuwa mkuu wa chuo cha Tiba Lugalo (MCMS) kuchukua nafasi ya Brigedia Jenerali Msangi anatestaafu leo kazi baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria .Kabla ya uteuzi Brigedia Jeneral Mwanjela alikuwa mkuu wa Tiba Hopsitali kuu ya Jeshi Lugalo.
 
Aidha,Rais Magufuli amemteua Brigedia Jeneral George Msongole kuwa   Kamanda wa Brigedia ya Tembo  kuchukua nafasi ya Brigedia Jeneral J.M Chacha ambaye anastaafu leo  kisheria baada ya kufikisha umri wa kustaafu,.Bregedia Jenerali Msongole kabla ya kustaafu alikuwa Afisa Mnadhimu makao makuu ya Jeshii.
 
Rais Magufulia pia amemteua  Bregedia Jenerali Sylevesta M.Minja kuwa mkuu wa chuo cha ukamanda  kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Ezekiel Kyunga ambaye anastaafu kazi  leo baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria ambapo kabla ya uteuzi,Bregedia Jenerali Minja alikuwa mkuu wa utawala katika chuo cha Ulinzii wa Taifa –NDC.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MAWENZI MKOANI KILIMANJARO

Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Majaliwa Kassim Majaliwa akiwasili Ikulu ndogo ya mjini Moshi.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akisalimiana na Waziri mkuu  Majaliwa.
Waziri Mkuu  akislimiana na Mstahiki meya wa  Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya .
Waziri mkuu akiwasili katika hosiptali  ya rufaa ya Mawenzi alipofanya ziara  ya  kushtukiza.
Waziri mkuu akitizama chumba cha kupigia  pcha za mionzi (X Ray) katika hospitali  ya rufaa  ya Mawenzi.
Waziri mkuu akiwa wodi ya watoto alipotembelea kujionea namna ambavyo  wagonjwa wanahudumiwa.
Waziri mkuu Majaliwa akizungumza jambo na mganga  mkuu wa mkoa  wa Kilimanjaro, Dkt Mtumwa  Mwako.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akitoa taarifa ya mkoa kwa Waziri  mkuu  Kassim Majaliwa.
Wakuu wa wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika mkutano huo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Vunjo , Mhe. James Mbatia walipokutana Ikulu ndogo mjini Moshi.
Baadhi ya Viongozi walifika Ikulu ndogo mjini Moshi kwa ajili ya kumsikiliza ,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Na Dixon Busagaga wa Globu 

ya Jamii kanda ya Kaskazini.

Good News: Diamond Platnumz kazinyakua tuzo nyingine kubwa usiku wa leo.

Mmiliki wa hit song ya ‘UtanipendaDiamond Platnumz amezidi kuziandika headline katika ulimwengu wa sanaa baada ya usiku wa leo kuzinyakua tuzo mbili za Hipipo Awards zilizofanyika Uganda.
Ushindi alioupata ni Nyimbo bora Afrika Mashariki na Video bora Afrika Mashariki ambazo zote ni kupitia wimbo wa Nana.
Baada ya ushindi kupitia account yake ya Instagram Diamond aliandika maneno haya
MONDDDDDDDDDDD
Wow! Realy wanna Thank GOD for keep blessing the innocent kid… also wana thank all Media and My Loyal fans for the Big love.. Two Awards tonight on @HipipoAwardsUGANDA…EAST AFRICA SUPER HIT#NANA and EAST AFRICA BEST VIDEO#NANA many thanks to my brother@2niteflavour
@i_am_godfather and all Behind this Hit!!!… thanks alot @HIPIPOAwards for keep supporting the real African talent!
(Wadau kijana wenu nimefanikiwa kushinda tunzo mbili Usiku wa leo kama NYIMBO BORA AFRICA MASHARIKI#NANA na VIDEO BORA AFRICA MASHARIKI #NANA nawashkuru sana kwa kura na support zote mnazoendelea kunipa….. tafadhali nisaidieni kuhesabu ni tunzo ngapi tumechkua tangu Mwaka 2016 uanze? ) shukran sana

Haya ndo Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo January 31 2016