Diamond Platnumz kuingia kwenye jumba la BBA Hotshots leo (Nov 27) kupiga story na washiriki
Diamond Platnumz tayari ametua jijini Johannesburg, Afrika Kusini
toka jana, tayari kuhudhuria tuzo za Channel O (CHOAMVA) zinazotarajiwa
kutolewa siku ya..> Jumamosi Nov.29 akiwa anawania vipengele vinne.
Staa huyo ambaye ameachia ngoma mpya siku chache zilizopita ‘Ntampata
wapi’, ameandika kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamaii kuwa pia
leo Alhamisi Nov.27 atapata nafasi ya kuingia kwenye jumba la Big
Brother kubadilishana mawazo na washiriki.
“Tafadhali usikose kuangalia Big Brother Afrika kuanzia saa tano
Asubuhi kesho (leo), kijana wako Platnumz ntakuwa ndani ya nyumba
nikizoza mawili matatu na washiriki….” aliandika Diamond.
No comments:
Post a Comment
paulmkale