Tazama Picha: Mkubwa na Wanawe yatoa msaada kwa kituo cha watoto yatima Temeke
Katika kusherehekea kutimiza mwaka mmoja wa Yamoto Band, kituo cha
Mkubwa na Wanawe leo kimekabidhi msaada kwenye kituo cha watoto yatima
kilichopoa Temeke, Dar es Salaam.
Akikabidhi msaada huo, mkuu wa kituo hicho, Said Fella alisema: Kabla
ya kuzungumza chochote Napenda kutoa shukrani zangu kwa Mwenyezi Mungu
kwa kila jambo ambalo limefanikiwa ni kwa kupitia yeye aliye muweza wa
yote.”
“Pili nawashukuru Watanzania wote karibu kila nyanja kwa kuonyesha
ushirikiano wao kwa Mkubwa na Wanawe mpaka kufikia hapa hii leo.Toka
ianzishwe Yamoto Band leo ni siku ya furaha kwetu kusheherekea mwaka
mmoja ambao umefanyika kuwa na mafaanikio mengi makubwa. Moja kati ya
mafanikio hayo ni kuuza kazi zetu kweye mtandao na kukuletea kokote
ulipo mpaka majumbani,” alisema.
Aliongeza: Na kwa hiki kidogo tulichokipata sisi ukijumuisha na
furaha tuliyo nayo ya kutimiza mwaka mmoja tumeona ni bora tugawane na
wenzetu ambao ni wahitaji haswa kwa msimu huu wa sikukuu kama
tulivyozoea kufanya toka kipindi cha nyuma kwani hawa ni sehemu yetu
kama wanajamii wenzetu.Na kwa wale wapenzi na mashabiki wa Yamoto Band
tupo tayari kukupatia kilicho bora zaidi.
No comments:
Post a Comment
paulmkale