Mbunge
wa Mbinga Mh. Kapten John Komba amefariki dunia leo saa kumi jioni
katika hospitali ya TMJ Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa mtoto wa marehem Jerry Komba,amesema kifo cha marehemu baba
yake kimetokana na ugonjwa wa kisukari ambapo amedai kuwa sukari
ilishuka ghafla akiwa nyumbani kwake Mbezi Beach.
Miaka
mitatu iliyopita, Komba alipelekwa nchini India alikokwenda kufanyiwa
upasuaji kwenye nyonga, tatizo lililomsumbua kwa muda mrefu likichagizwa
na ule unene aliokuwa nao.
Katibu wa mbunge Gasper Tumaini alisema kuwa mbunge huyo alikimbizwa katika hospitali ya TMJ na ndipo mauti yalipomkuta.
Katibu
huyo alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hosp ya Lugalo
jijini Dar Es salaam ambapo ratiba ya maziko bado haijafahamika.
No comments:
Post a Comment
paulmkale