Mwanamuziki wa kundi la Weusi, Nikki wa Pili amefunguka kuja na kampeni
ya ‘Uchaguzi kwa Amani’ ili kuweza kuwahamasisha vijana kushiriki
uchaguzi mkuu kwa amani.
Akihojiwa amesema kuwa wazo hilo limemjia baada ya kuona tangu mwaka
1995 vurugu zimechukuliwa kama sehemu ya kampeni hivyo kampeni hiyo
itasaidia kuwahamasihsa watanzaniakushiriki uchaguzi wa 2015 kwa amani.
Amesema kuwa tangu mwaka 1995 watu wamekuwa wakihamasishwa kushiriki
katika uchaguzi kupata haki ya kupiga kura lakini hakuna kampeni
zilizofanywa za kuwaelimisha changamoto za vurugu na kuongeza kuwa kwa
kuwaelimisha kutawasaidia sana kufanya uchaguzi wa amani.
Amesema kuwa walengwa wakubwa wa kampeni hiyo watakuwa ni vijana kwahiyo
wataanza kuongea na vijana wenzao kuwa demokrasia ni malumbano ya hoja,
siyo malumbano ya vikundi, kwa hiyo wasimtazame mtu na chama chake,
bendera yake, na kuongeza kuwa mtu atazamwe kwa hoja na ajibiwe kwa
hoja.
Amesema wameshaanza kuhamasisha kupitia mitandao ya kijamii na
wameshaanza kutoa makala kwenye maazeti, mahojiano kwenye redio na
endapo wahisani wakitokea watatembea nchi nzima
No comments:
Post a Comment
paulmkale