MASIKINI DIAMOND PLATNUMZ ANUSURIKA KUKATWA MGUU... ANGALIA VIDEO YA TUKIO ZIMA HAPA
Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya na nyota wa Wimbo wa Nitampata
wapi aliyewahi kuwa mchumba wa Wema Sepetu, Nasibu Abdul ‘Diamond’
amenusurika kukatwa mguu katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar
es Salaam kufuatia ugonjwa wa Foot Corn (maarufu kwa jina la kisahani)
kumtesa kwa kipindi kirefu.Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya na nyota wa Wimbo wa Nitampata, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Diamond ambaye kwa sasa anaminya
kimalavidavi na mwanamama Zarina Hassan ‘Zari’, alianza kusumbuliwa na
ugonjwa huo takribani siku 730 zilizopita (miaka miwili), huku mwenyewe
akipuuzia matibabu yake na kuelekeza nguvu kwenye shoo za ndani na nje
ya nchi. “Mara kwa mara alikuwa akilalamikia maumivu makali ya mguu lakini kwa
kuwa yalikuwa yakija na kupotea, alikuwa akipuuzia kwenda hospitali
mpaka juzi (Ijumaa) alipoamua kwenda TMJ,” kilisema chanzo chetu kwa
masharti ya kutotajwa jina.
WALICHOKIBAINI MADAKTARI
“Madaktari
walipompima, walishangazwa na jinsi alivyokuwa amechelewa kwenda kupata
matibabu, nasikia ugonjwa aliokuwa nao ni hatari sana. Kama angeendelea
kuchelewa, huenda wangelazimika kumkata mguu kabisa, Diamond aliogopa
sana,” kilisema chanzo hicho.
Ikazidi kuelezwa kuwa baada ya vipimo
kukamilika na kubainika kuwa alikuwa na Foot Corn, madaktari walimueleza
kuwa ni lazima wamfanyie upasuaji wa haraka wa kutoa nyama zilizokuwa
zimeota kwenye mguu wake ambazo zilitengeneza kitu kama kisahani.
NDANI YA CHUMBA CHA UPASUAJI
Baada
ya taratibu zote kukamilika, Diamond aliingizwa ndani ya chumba cha
upasuaji ambapo jopo la madaktari kadhaa, wakiwemo wenye asili ya Bara
la Asia walimfanyia upasuaji.
SHOO NYINGI ZILISABABISHA ACHELEWE MATIBABU
Kwa
mujibu wa chanzo kingine ambacho ni ndugu wa msanii huyo, sababu
iliyosababisha Diamond akachelewa kwenda hospitali kutibiwa tatizo hilo,
ni kubanwa na shoo nyingi ambapo alikuwa akihofia kwamba akienda
hospitali anaweza kulazwa au matibabu yakachukua muda mrefu hivyo
kuvuruga mikataba ya shoo ambayo tayarti alikuwa ameshasaini.
MSIKILIZE DIAMOND
Baada
ya kukamilika kwa upasuaji huo, mwanahabari wetu aliyekuwa akifuatilia
tukio zima kuanzia mwanzo hadi mwisho, alizungumza na Mbongo Fleva huyo
ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Nawashukuru sana madaktari wa TMJ kwa kuweza kufanikisha upasuaji huu,
Mungu awabariki sana. Ugonjwa ulianza kama miaka miwili hivi iliyopita
lakini nilishindwa kufanya upasuaji kwani shoo zilikuwa zinabana, safari
hii nikaona bora tu nifanye maana niliambiwa nikiacha tatizo linaweza
kuwa kubwa zaidi,” alisema Diamond.
MSIKIE DAKTARI BINGWA WA UPASUAJI
Ijumaa
Wikienda halikuishia hapo, lilimtafuta Dk. Edward Wayi, Daktari Bingwa
wa Upasuaji wa Hospitali ya CCBRT ambaye pia huzunguka katika nchi
mbalimbali za Afrika kutibu watu ambapo aliufafanua ugonjwa huo
kitaalamu.
“Ugonjwa wa Foot Corn unapokuanza, dalili za awali ni maumivu makali ya mguu ulioathirika.
“Ugonjwa usipotibiwa, husababisha malengelenge ambayo hupasuka na
kusababisha kidonda. Kidonda hicho kisipotibiwa, husababisha kuharibika
kwa ngozi ya ndani ya mguu inayotenganisha mifupa ya mguu na ngozi ya
ndani. Hali hii kitaalamu huitwa Bursitis.
“Mgonjwa akishafikia hatua hii, huwa kwenye hatari ya kupata tatizo
lingine kubwa zaidi liitwalo Septic Arthritis ambapo bakteria huingia
ndani ya mwili kwa kupitia kidonda, kusambaa kwenye mfumo wa damu na
kwenda kujikusanya kwenye viungio vya mifupa (joints).
“Mgonjwa akifikia hatua hii, viungio vya mifupa huvimba na kupata
maumivu makali mithili ya mtu anayechomwa na sindano au msumari. Hata
hivyo, kwa kuwa maumivu huwa yanakuja na kukata, wengi hupuuzia na
matokeo yake, ugonjwa huingia kwenye hatua ya hatari zaidi iitwayo
Osteomyelitis.
“Katika hatua hii, bakteria huwa tayari wamepanda na kuingia ndani ya mfupa kisha kuanza kuushambulia kwa kasi.
Mgonjwa
akishafikia hatua hii, huwa hakuna tiba nyingine zaidi ya mguu kukatwa.
Nawashauri Watanzania kutopuuzia ugonjwa huu kwani tayari watu wengi
wameshakatwa miguu kwa sababu ya kuchelewa kupata matibabu,”
alihitimisha daktari huyo.
No comments:
Post a Comment
paulmkale