Meninah : Sitembei na Barakah Da Prince Kuna Project Tunaandaa

Mwanadada wa Muziki mwenye Umbo la aina yake Amekanusha taarifa Zilizozagaa Kwamba ana Mahusiano ya Kimapenzi Na Nyota Toka Mwanza Staa Wa “Siachani Nawe “baraka Da Prince,Meninah amesema kuwa kweli amekuwa akionekana kwa karibu  na msanii huyo lakini ifahamike kinachowaweka karibu ni kazi yao ya muziki


“Sitembei na Barakah ,kwa sababu Baraka ni Kama Mdogo wangu ,najuana nae toka hajaanza Muziki hata mimi nilikuwa sapoti yake kubwa katika kumshauri hivi na vile kuhusu muziki,so Kuna project yetu na itatoka ya kwangu mimi na yeye kuna song ameniandikia ambayo tayari nimeishaifanya na ippo tayari ,kukaa na mtu karibu sio kwamba unatoka nae jamani nilikuwa nae sana karibu,Tulikuwa tuna studio session nilikuwa nampitia kwao lakini sio kwamba niko nae”Alimalizia Menina

No comments:

Post a Comment

paulmkale