Ushauri wa Bure Kwa Ali Kiba Baada ya Kutoa Wimbo Mpya, Tafuta Watu wa Kukutungia Nyimbo
Anyways, leo nimepata chance ya kusikiliza nyimbo mpya ya Ali Kiba fasta fasta….
I like Ali Kiba’s music but I think he needs to grow kimuziki. Mie naona
toka arudi kwenye gemu nyimbo zake zimeshuka kiwango sio nzuri kama za
zamani… Au labda tuseme yani nyimbo zake zote ni vile vile yani hazina
tofauti.Yani they sound identical.Anabadilisha vitu vidogo vidogo sana……
Nyimbo zake za zamani zilikuwaga nzuri sana , ila pia yawezekana za
sasa hivi zinaoneka sio nzuri sababu zimefanana na za zamani…Yani nyimbo
ya Ali Kiba hata uamshwe usingizini bila kusikia hata sauti ukisikia
biti tu unajua nyimbo ya Ali Kiba….lol….
Kwenye issue ya kiwango cha nyimbo kushuka hayuko peke yake hata besti
ake Diamond pia nyimbo zake zimeanza kushuka kiwango…. Mie naona tatizo
lipo hapa…. Ni kwamba wamesha maliza material zao zooooote nzuri…. Ni
sawa na kwenye mashindano ya kukimbia unapoanza kukimbia unakimbiaje
fastaaaaa kama gari vile, ila mwisho wa mashindano nguvu zinaisha
unaweza hata anza tembea…Mie naona ndo kama hawa vijana, wameshaandika
all the best stuff they have sasa material zimekwisha inabidi wafanye tu
ili mradi watoe new single….
Yani kwa Ali Kiba kwa jinsi alivyo under pressure sababu ya hiyo ya
likinganishwa na Diamond naona hii new single imemwangusha kabisa yani
na sasa ni dhahiri kuwa yeye ni number 2.
Well, kunapokuwa na tatizo lazma tutafute na suluhisho… Tumeshajua
tatizo sasa hivi ni unandishi wa nyimbo sio kwamba hawajui kuimba kama
zamani. Talent zao zipo pale pale au hata labda zimeongezeka kutokana na
experience ila problem is hawana tena material ya kuandika nyimbo. I
think hata VANESSA MDEE na JUMA JUX wanaface the same problem.
Yani Vanessa na Juma Jux wana swaga za hatariiiiiiiii, yani wamekaa
kimamtoni ile mbayaa ila tatizo ni nyimboooooooo, nyimbo hazina viwango
vileeeee…..Well wafanyaje sasa???
I think hapa mie nimeona kuna fursa kubwa sana ya uandishi wa nyimbo Yes
asilimia kubwa ya artists wengi wa marekani huwa wanaandikiwa nyimbo
zao. Especially baada ya kuwa kwenye gemu for a while maana na wao huwa
wana run out of material au aideas ndo hapo inabidi wanunue..
Kwa mfano one of the most popular hits in the world ule wa I will always
Love you wa Whitney Houston – yeye aliununua tu,ule wimbo uliandikwa na
mtu mwingine. I think uliandikwa na Dolly Parton. So kama Whitney
angetaka sifa za kujifanya yeye anajua kuimba na kuandika songs zake
mwenywe basi sidhani kama angejulikana dunia nzima kama alivyojulikana
baada ya huo wimbo alioununua kwa Dolly Parton. Au tuseme Michael
Jackson, mnaikumbuka ile nyimbo yake ya Thriller wakati tuko watoto
tulikuwa tunaipenda balaaaa, na ilikuwa number 1 hit all over the world.
Guess what Michael Jackson hakuandika ule wimbo aliununua kwa mtu
anaitwa Rod Temberton.
Yani kuna watu wanakuwa mamilionea kwa kuandikia waimbaji nyimbo. So
jamani mie naona its time sasa watokeee professional song writters
Tanzania waanze kuwaandikia hawa waimbaji wetu nyimbo. Kama sio hivyo
ndo hivyo wataendelea kutoa nyimbo zisizo na viwango mpaka mwisho
watasahauliwa maana kuna new artisits ambao wana nyimbo zao mbili tatu
kaliiiiii watatoa tutawapenda then tutawasahau hawa.
Kama wanataka kubaki on top of the game for many years inabidi waanze kununua nyimbo sasa.
Source: U-turn
No comments:
Post a Comment
paulmkale