Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa
Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuashiria
uzinduzi wa Skuli ya Msingi Mnarani leo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa
Kaskazini Pemba iliyojengwa kwa Nguvu za wananchi na Ufadhili ya
Shirika la Milele Foundation la Zanzibar,ufunguzi huo ikiwa katika
shamra shamra za kusherehekea miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar(kulia) Katibu Mkuu Wizra ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Bi.Khadija Bakari na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma
Shamuhuna (kushoto) ,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa
Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kuashiria ufunguzi
wa Skuli ya Msingi Mnarani leo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini
Pemba iliyojengwa kwa Nguvu za wananchi na Ufadhili ya Shirika la
Milele Foundation la Zanzibar,ufunguzi huo ikiwa katika shamra shamra za
kusherehekea miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na
Ikulu.]
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa
Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanafunzi
mara baada ya kuifungua na kuitembelea Skuli ya Msingi Mnarani Wilaya
ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo,iliyojengwa kwa Nguvu za
wananchi na Ufadhili ya Shirika la Milele Foundation la Zanzibar, ikiwa
katika shamra shamra za kusherehekea miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
Wanafunzi wa Skuli ya Msingi
Mnarani Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakimsikiliza Rais
wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein
wakati alipokuwa akizungumza nao baada ya kuifungua rasmi leo ikiwa ni
katika sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar, [Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa
Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea Risala kutoka kwa
Mossi Hamadi Khamis katika sherehe ya ufunguzi wa Skuli ya Msingi
Mnarani Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba iliyojengwa kwa
ushirikiano wa Serikali,Nguvu za Wananchi na Shirika la Milele Zanzibar
Foundation leo ikiwa ni katika sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, [Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa
Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wananchi, pamoja
na viongozi mbali mbali waliohudhuria katika ufunguzi wa Skuli ya Msingi
Mnarani Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo iliyojengwa
kwa ushirikiano wa Serikali,Nguvu za Wananchi na Shirika la Milele
Zanzibar Foundation ikiwa ni katika sherehe za maadhimisho ya miaka 52
ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, [Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa
Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu
Wizra ya Elimu na Mafunzo ya Amali Bi.Khadija Bakari wakati alipowasili
viwanja vya Skuli ya Msingi Mnarani Wilaya ya Micheweni kuifungua Skuli
hiyo iliyojengwa kwa Nguvu za wananchi na Ufadhili ya Shirika la Milele
Foundation la Zanzibar leo ikiwa katika shamra shamra za kusherehekea
miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
……………………………………………………………………………………..
Na Ali Issa Maelezo –Zanzibar
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi
na Utumishi wa Umma Haruon Ali Suleiman ameshauri walimu
watakaosomesha Skuli ya Zingwezingwe wawe walimu wanaoishi karibu na
kijiji hicho.
Hayo ameyasema leo huko
Zingwezingwe Mkoa wa Kaskazini, Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja, wakati
alipokuwa akifungua skuli mpya ya msingi ya kijiji hicho ikiwa ni
miongoni mwa shamra shamra za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar .Ametaka ushauri huo ufanyiwe kazi
na iwapo watahitajika walimu wapya kuajiriwa kwa ajili ya kufundisha
katika skuli hiyo Wizara yake ambayo ndiyo inayohusika na masuala
ya ajira watakuwa tayari kufanya hivyo.
“Ni vyema kuajiri walimu wakaazi
na wenyeji wa kijiji cha Zingwezingwe wenye kuyaelewa mazingira ya
kijiji hicho na mimi kama Waziri wa Ajira niko tayari kusaidia hilo,”
alisema Waziri Haroun.Aidha aliwashauri wanafunzi
wanaosoma katika skuli hiyo kuitumia frusa waliyoipata kusoma kwa
juhudi kwani hiyo ni skuli ya kwanza kujengwa katika kijiji hicho.
Hata hivyo aliwataka wazazi na
walezi kwa upande wao kutimiza wajibu wao wa kufuatilia kikamilifu
maendeleo ya Watoto wao na kutoa ushirikiano kwa walimu ili
kufanikisha maendeleo ya watoto wao.
Waziri Haroun aliwataka walimu
kusomesha kwa juhudi kwani serikali tayari imeshatoa maelekezo ya
kuwaongezea maslahi yao mara itakaporudi madarakani baada ya uchaguzi
wa marejeo.Katika kuongeza ujenzi wa
madarasa mengine ya kusomea katika Skuli hiyo, Waziri wa Nchi Afisi ya
Rais Kazi na Utawala wa Umma alichangia matofali 1000 ambapo ujenzi
wake utaaza hivi karibuni.
Nae Mke wa Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Mama Asha Balozi akitoa salamu za Baloz Seif Ali Idd
alisema suala la umeme katika skuli hiyo litafanywa na Makamu huyo wa
Rais.
Ujenzi wa skuli hiyo yenye
madarasa manne na Ofisi ya Mwalimu Mkuu umegharimu shilingi milioni 66
ambazo zimetolewa na Shirika la Maendeleo la Sweden SIDA, Halmashauri
ya Wilaya ya Kaskazini B, Mbunge na Mwakilishi na Wazee wa kijii cha
Zingwezingwe.
No comments:
Post a Comment
paulmkale