Shirika
la ndege la bei nafuu lapanua wigo wa safari zake barani Afrika na
kufungua safari ya kimataifa ya moja kwa moja kutoka Nairobi kwenda Dar
es Salaam na Kilimanjaro.
Januari 2016
– fastjet imetangaza safari yake mpya ya kimataifa ya kutoka Dar es
Salaam kwenda Nairobi, Kenya kuwa itaanza rasmi mnamo tarehe 11 Januari
2016.
Fastjet
imepewa ruhusa na serikali ya Kenya kufanya safari zake nchini humo
kufuatia makubaliano ya pamoja na mashirika yanayotoa huduma za usafiri
wa anga kati ya nchi hizi mbili za Tanzania na Kenya, kama
ilivyopitishwa na serikali ya Tanzania.
Vilevile
Fastjet imetangaza kuwa inatarajia kuzindua safari zake za anga kati ya
Zanzibar na Nairobi na pia kati ya Dar es Salaam na Mombasa ambapo
uzinduzi huo utafanyika mapema mwaka huu 2016.
Tiketi
za kurudi kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini
Nairobi kwenda uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
na uwanja wa ndege wa Kilimanjaro zitakuwa za kila siku mara tu baada ya
uzinduzi huo na wasafiri watasafiri na ndege ya kisasa aina ya Airbus
A319 ambayo hubeba abiria 156.
Kwa
mujibu wa Fastjet, safari nyingine za ndege zinatarajia kuzinduliwa
kufuatia kuongezaka kwa maombi ya wateja wake na hii ni kwa sababu ya
unafuu wa bei zake sambamba na huduma bora.
Tiketi
za safari hii mpya zimeanza kuuzwa, na nauli za Nairobi/Dar es Salaam
zitatozwa kwa $50 kwa safari moja, na Dar es Salaam/ Nairobi zitatozwa
kwa $80 kwa safari moja.
Nauli
hizi ni pamoja na kodi ya serikali ambayo itachajiwa. Kwa mantiki
hiyo, Fastjet inawaomba abiria na wateja wake kwa ujumla kufanya booking
mapema iwezekanavyo ili kufaidika na bei nafuu ambayo hutozwa kuliko
ndege zote ambazo husafirisha abiria kati ya nchi hizi mbili.
“Usafiri
wa anga katika uwanda wa Afrika mashariki umekuwa na ushindani mkubwa
kutokana na safari nyingi bado hutoza nauli kubwa jambo linalosababisha
abiria wengi kushindwa kumudu safari hizo” alisema John Corse, Meneja
Mkuu wa fastjet kanda ya Tanzania.
“Wasafiri
wengi wanaosafiri kati ya miji hii miwili mikubwa yenye idadi ya watu
wasiopungua milioni 8 hapa Afrika Mashariki wamekuwa wakipatwa na vikazo
mbalimbali vinavyowarudisha nyuma kutokana na bei ya safari za ndege
kuwa kubwa ambayo tunaamini imewakatisha tamaa wasafiri wengi”, alisema
Corse.
Matarajio
ya Fastjet kufanya safari zake nchini Kenya zitaleta matumaini mara tu
baada ya shirika hilo kuzindua safari hizo ambazo bei zake zimepokelewa
na wateja wengi wanaosafiri na ndege zingine hasa pale ambapo nauli za
Fastjet zimepungua kwa asilimia 40 hivi.
“Jambo
kuu la msingi ni kwamba ushindani ni muhimu kwa wateja, kwa kuwa inampa
mteja nafasi ya kuchangua unafuu wa nauli atakayoimudu, na hali hii
hufanya watalii na wajasiriamali na wageni wanaotembelea nchi hizi mbili
kuwa huru kuamua kwa raha kati ya Tanzania na Kenya” Corse alisema.
“Hali
hii baadae italeta maendeleo ya pamoja kati ya nchi hizi mbili ambapo
ukuwaji wa biashara zao za ndani na nje, vilevile pia utalii utaimarika
kwa kiasi kikubwa na itakayo pelekea kukua kwa uchumi wa nchi hizi
mbili”, aliongeza Corse.
Pia
alisisitiza kuwa haileti maana halisi kwa mgeni ama mtalii kusafiri kwa
zaidi ya masaa 12 kutoka Dar es Salaam kwenda Nairobi Kenya na kumfanya
achoke kama ilivyo katika safari zingine. Na kwa kuwa sasa Fastjet
imezindua safari mpya kama hii ya nchi na nchi, basi inategemea wasafiri
wengi watafaidika na huduma za Fastjet.
Kwa
kuunga mkono mategemeo haya hapo baadae, hii ni baada ya Fastjet
kufanya utafiti wa kina na kubaini kuwa abiria wake waliweza kumudu bei
zao na kuzikubali moja kwa moja.
Safari za kila siku za fastjet kutoka Dar es Salaam zitaanza saa 3:50 asubuhi na kutua Nairobi-Kenya saa 5:10.
Safari za kurudi kutoka Nairobi kwenda Dar es Salaam zitaanza saa 8:10 na kutua saa 10 :05 kulingana na saa za Afrika mashariki.
Safari
za kwenda Kilimanjaro kutoka Nairobi zitaanza saa 5:10 na kutua saa
6:40 na safari ya kurudi kutoka Kilimanjaro kwenda Nairobi zitaanza saa
7:10 na kutua saa 8: 40 kulingana na saa za Afrika mashariki.
Fastjet
inatoza nauli iliyo nafuu kadri iwezekanavyo na kwa kutozingatia
gharama za ushuru wa mizigo, vinywaji lakini vyote hivi vinapatikana
kama msafiri atagharamia kwa hiari yake mwenyewe.
Ukatishaji tiketi mapema unaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kwa kupitia tovuti ya festjet ambayo ni www.fastjet.com
kupitia kwa mawakala wa shirika hili, ama mteja anaweza kupiga simu
Namba 0784 108900. Malipo kwa ajili ya tiketi yanaweza kufanyika taslimu
ama kwa kutumia benki ama kwa njia ya mitandao ya simu za mikononi.
Fastjet
imepanua wigo wa ofisi zake na kwa sasa wanaendesha shughuli zao
kimataifa kati ya Dar es Salaam ambako ndiyo ofisi kuu na kushirikiana
na Johannesburg Afrika Kusini, Lusaka-Zambia, Entebbe - Uganda,
Harare-Zimbabwe na Lilongwe nchini Malawi. fastjet pia hufanya safari
zake kwenda Entebbe.
Fastjet
pia hufanya safari zake za ndani ya nchi kutoka Dar es Salaam kwenda
Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro na pia kati ya Kilimanjaro na Mwanza. Safari
ya kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar itaanza tarehe 11th Januari
2016.(P.T)
No comments:
Post a Comment
paulmkale