Kansela Angela Merkel akizungumzia mkutano wa chama chake cha CDU alipokutana na waandishi wa habari. (09.01,2016)
Kansela
Angela Merkel amesema Jumamosi (09.01.2016) kwamba anataka kuwepo kwa
sheria kali za uhamiaji nchini Ujerumani baada ya mashambulizi kadhaa ya
ngono mjini Cologne na katika miji mengine kulifadhaisha taifa
Akizungumza
baada ya mkutano miongoni mwa viongozi waandamizi wa chama chake cha
Christian Demokrat (CDU) mjini Mainz Merkel amesema " Kile kilichotokea
katika mkesha wa mwaka mpya ni vitendo vya uhalifu vya kukirihisha
ambavyo vinahitaji kuchukuliwa hatua kali."
CDU
mojawapo ya chama tawala nchini Ujerumani imechukuwa hatua hiyo ya
kuimarisha sheria ya waomba hifadhi kufuatia mashambulizi makubwa ya
ngono dhidi ya wanawake katika mkesha wa mwaka mpya mjini Cologne.
Chama
hicho kimelipa kipaü mbele suala la kuharakisha kurudishwa makwao
watafuta hifadhi wanaotenda uhalifu nchini katika mpango wao vipengele
kumi juu ya mustakbali wa Ujerumani.
Rasimu ya
mpango huo wa CDU inajumuisha sheria mpya ambayo itamvuwa mhamiaji
hadhi ya kupatiwa hifadhi baada ya kufanya kosa moja la uhalifu.
Hatua
hiyo yumkini ikazusha majibu ya moja kwa moja kutokana na taarifa kwamba
baadhi ya wanaume waliokamatwa kuhusiana na udhalilishaji wa kingono
mjini Cologne kwa kweli walikuwa ni wahamiaji wanaomba hifadhi ukweli
ambao ulifichwa kwa sababu za kisiasa.
Wakimbizi kupoteza haki ya ukaazi
Merkel
amesema "iwapo mkimbizi anavunja sheria lazima kuwepo na taathira yake,
hiyo ina maana wanaweza kupoteza haki yao ya ukaazi hapa nchini bila ya
kujali anakabiliwa na kifungo cha nje au cha gerezani."(P.T)
Ameongeza
kusema iwapo sheria haikidhi haja hiyo basi lazima ibadiishwe na
kusisitiza kwamba kuimarishwa huko kwa sheria sio tu kwa ajili ya
maslahi ya raia bali pia kwa maslahi ya wakimbizi walioko nchini.
Chini ya
sheria za hivi sasa waomba hifadhi wakipatikana na hatia wanaweza tu
kufukuzwa nchini iwapo wamehukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani na
isitoshe maisha inabidi yasiwe hatarini iwapo watarudishwa makwao.
Wafuasi wa PEGIDA waandamana
Mamia ya
wafuasi wa sera kali za mrengo wa kulia wamejitokeza Jumamosi katika
maandamano mjini Cologne kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kingono
dhidi ya wanawake vinavyodaiwa kufanywa na wahamiaji katika mji huo wa
Ujerumani magharibi wakati wa sherehe za mkesha wa mwaka mpya.
Wafuasi
wa vuguvugu la kundi la PEGIDA lenye kupinga kusilimishwa kwa Ulaya
walikuwa wakipiga mayowe ya kutaka kufukuzwa kwa wahamiaji na kebeba
mabango yenye ujumbe wakimbizi hawatakiwi.Mwanachama mmoja wa kundi hilo
aliuambia ummati kwamba Merkel amekuwa hatari kwa nchi yao na kwamba
lazima aondoke kauli yake hiyo ilikuwa ikirudiwa kuitikiwa na umati
uliomiminika hapo.
Waandamanaji
wa sera za mrengo wa shoto pia walifanya maandamano sambamba na hayo
kulipinga kundi hilo la PEGIDA wakiwapigia makelele kwa kuwaita Manazi.
Azimio la Mainz
Hata
hivyo mabadiliko yoyote yale ya sheria itabidi yajadiliwe na serikali ya
mseto ya Merkel ambayo pia inashirikisha chama cha SPD chenye baadhi ya
wanachama ambao tayari wameashiria kupinga marekebisho yoyote yale.
Mbali na
sheria "Mainzer Erklärung" yaani Azmio la Mainz linatowa wito wa
kuimarishwa kwa usalama katika maeneo ambayo mashambulizi mingi hutokea
kwa mfano kituo cha reli cha Cologne,kuweka kamera zaidi za video na
wanausalama kuwakaguwa watu kiholela.
Polisi ya
Ujerumani hadi sasa imewatambuwa watuhumiwa 32 ishirini na mbili kati
yao ni watafuta hifadhi na kuhusiana na makosa 76 kumi na mbili yakiwa
na sura ya dhila za ngono .
Chanzo:DW
No comments:
Post a Comment
paulmkale