Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAZIRI
wa Katiba na Sheria,Dk.Harrison Mwakyembe amesema kuwa suala la
kuanzisha mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi wanafanyia kazi na
muda sio mrefu watatoa taarifa juu ya hatua walizofikia.
Dk.Mwakyembe
ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Ofisi ya Mkurugenzi wa
Mashitaka nchini (DPP),amesema kuwa suala mahakama linafanyiwa kazi kwa
karibu na ofisi yake kutokana na ahadi ya Rais Dk.John Pombe Magufuli
wakati wa kampeni.
Mwakyembe
amesema kuwa watu ambao wanaweza kuleta maendeleo ya nchi ni vyombo
vilivyo katika maamuzi ya kisheria hivyo lazima viweze kufanya kazi kwa
wananchi kwa kutenda haki.
Amesema
kuwa baadhi ya watendaji wa taaluma ya sheria sio waaminifu kwa
kujihusisha na rushwa na kufanya watendaji wote kuharibika kwa sababu ya
mtu mmoja.
Mwakyembe
amesema yeye ni mwanasheria na kuongeza kuwa kuna’ majipu’katika tasnia
ya taaluma ya sheria na kuwataka majipu hayo yatumbuliwe kabla ya Rais
Dk.John Pombe Magufuli hajayatumbua bila sindano ya kupunguza maumivu
(Ganzi).
Mwakyembe
amesema kuwa wanajua changamoto ya mawakili wa serikali wanazokumbana
nazo ikiwemo miundombinu pamoja na mfumo wa maisha wanayoishi hivyo
serikali itafanya uwezeshaji kadri ya uwezo wao.
Mkurugenzi
wa Mashitaka nchini,Buswello Mganga amesema katika mafanikio
walioyapata ni pamoja kushinda kesi nane za dawa za kulevya kwa
watuhumiwa kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 hadi 30.
Mkurugenzi
wa mashtaka nchini, Biswelo Mganga akizungumza na kueleza mbambo
mbalimbali mbele ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe
na kazi walizozifanya ikiwa ni pamoja na kuwashataki wenye hatia za
uuzaji na usafirishaji wa madawa ya kulevya.
Waziri
wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na watendaji
wa Ofisi ya Mwendesha mastaka nchini (DPP) na baadhi ya Waandishi wa
Habari kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Sheria ikiwemo majumuisho ya
ziara ya Sheria na Katiba aliyoifanya hivi karibuni Jijini Dar es
Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Sheria na Katiba ,Amon Mpanju akizungumza na waandishi
wa habari leo jijini Dar es Salaam mara baada ya Waziri wa Katiba na
sheria kufanya ziara na kujifunza mambo mbalimbali katika ofisi ya
mwendesha mashtaka (DPP).
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Profesa Sifuni Mchome akizungumza
na wadau wa sheria pamoja na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
leo.
Waziri
wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam leo. kutoka Kulia ni Naibu katibu mkuu wa
Wizara ya Katiba na Sheria, Suzan Mlai, Mkurugenzi wa mashtaka nchini, Biswelo Mganga na kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Sheria na Katiba, Amon Mpanju na Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Profesa Sifuni Mchome.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa toka Waziri wa Katiba na
Sheria pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka (hawapo pichani) leo 5 Januari,
2016 Jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
No comments:
Post a Comment
paulmkale