Tunakanusha
taarifa iliyochapishwa na gazeti la The Citizen la Januari 5, 2016
katika ukurasa wake wa 12 yenye kichwa cha habari: ‘Umma kununua
asilimia 49 ya hisa za Tanesco’. Mwandishi na Mhariri wamejiandikia
taarifa hiyo kwa sababu wanazozijua wao.
Sehemu ya taarifa inasema: Serikali ya Tanzania ina mpango wa kuuza hisa ya Shirika la Umeme Tanzania kwa umma...
Pia,
sehemu nyingine inasema: Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo
aliliambia gazeti la East African kuwa Serikali itatoa asilimia 49 ya
hisa za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakati huo Serikali ikibaki
na hisa zingine...
Tungependa wananchi kwa ujumla waelewe kwamba taarifa hiyo si sahihi na inapotosha umma. Taarifa sahihi kama ifuatavyo:
· Kwanza,
Waziri Sospeter Muhongo hajafanya mahojiano yoyote na mwandishi wa
gazeti hilo la The East African wala gazeti la The Citizen.
· Pili, Serikali haina mpango wa kuuza hisa za TANESCO kwa umma.
Mkakati
uliopo wa Mageuzi ya kuboresha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
ujulikanao kama Electricity Supply Industry Reform Strategy and Roadmap
(ESI-RSR) 2014 – 2025 ni kama ifuatavyo:
MAELEZO YA MKAKATI NA MWELEKEO WA KUREKEBISHA SEKTA NDOGO YA UMEME (ESI-RSR)
Mwezi
Juni 2014, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipitisha na
kuchapisha mkakati wa mageuzi wa Electricity Supply Industry Reform
Strategy and Roadmap (ESI-RSR) 2014 – 2025. Lengo la msingi wa mkakati
huo ni kuboresha mazingira ya uwekezaji wa sekta binafsi katika nyanja
za uzalishaji na usambazaji, na kuongeza uunganishaji wa umeme katika
ngazi zote.
Utekelezaji
wa mpango huo ambao unatarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka
kumi na moja (11) umegawanyika katika vipindi vikuu vitatu ambavyo ni
muda mfupi, wa kati na muda mrefu.
Ø Mkakati
wa muda mfupi ni kutenganisha shughuli za Uzalishaji ili zifanywe na
Kampuni Tanzu ya TANESCO. Umiliki wa uzalishaji, usafirishaji na
usambazaji chini ya awamu hii itaendelea kuwa chini ya Serikali, kama
mbia moja.
Ø Mkakati
wa muda wa kati unahusu kutenganisha sehemu ya usambazaji kutoka kwenye
usafirishaji. Katika Awamu hii, Kampuni za uzalishaji, usafirishaji na
usambazaji zitaendelea kuwa chini ya umiliki wa Serikali.
Ø Mkakati
wa muda mrefu utahusishaOfisi za Kanda kujihusisha na usambazaji wa
huduma za umeme ambazo pia zitagawanywa kulingana na uwezo wa
kujiendesha. Katika kipindi hicho cha muda mrefu, kampuni binafsi za
usambazaji umeme zitaendelea kushiriki katika shughuli za uzalishaji na
usambazaji umeme kwa ajili ya kuchochea ushindani na ufanisi kwenye
soko.
Tunawahimiza
wadau wote kusoma mkakati wa mageuzi ujulikanao kama Electricity Supply
Industry Reform Strategy and Roadmap (ESI-RSR) 2014 – 2025 ambao
unapatikana mitandaoni
Aidha,
tunawakumbusha Waandishi wa Habari na Wahariri ambao hawazingatii
maadili ya taaluma yao kuandika taarifa sahihi ili kuepusha upotoshaji
kwa umma.
Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
6 Januari, 2016
No comments:
Post a Comment
paulmkale