Baadhi
ya Maafisa wa Wizara ya Afya na Wananchi waliohudhuria katika sherehe
za Ufunguzi wa Jengo la Hospitali ya Kivunge kwa Wagonjwa wa nje Wilaya
ya kaskazini A,Mkoa wa Kaskazini Unguja lililojengwa kwa ufadhili wa Shirika lisilo la kiserikali (HIPZ) kutoka Uingereza ikiwa ni katika shamra shamra za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 52
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame kwa
niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali
Mohamed Shein,akikata utepe kufungua Jengo la Wagonjwa wa Nje Hospitali
ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja lililojengwa
na Shirika lisilokuwa la kiserikali kutoka Uingereza (HIPZ) ikiwa ni
katika shamra shamra za Mapinduzi matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52
(wa pili kushoto) Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo Jecha
Viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na wananchi mbali mbali wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame Mwadini akitoa hutuba ya ufunguzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A.Unguja leo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Meneja
Mipango wa Shirika lisilolakiserikali kutoka Nchini Uingereza (HIPZ)
Bibi Pamela Allard akitoa salamu zake wakati wa ufunguzi wa Jengo la
Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A.Unguja
leo lililofunguliwa naWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame Mwadini ,kwa niaba ya Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame
(kushoto) pamoja na Viongozi wa Wizara ya Afya wakiangalia Uodhoreshaji
majina kwa wagonjwa wanaofika Hospitali kwa njia ya Mtandao baada ya kufungua
Jengo la Wagonjwa wa Nje Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A
Mkoa wa Kaskazini Unguja leo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, sherehe hizi ni katika
shamra shamra za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 52,(wa pili
kushoto) Dr,Alexander Vogt wa kujitolea wa Shirika la HIPZ kutoka
Uingereza
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame
Mwadini (kushoto) akimsalimia Mtoto aliyefika kupima Nazna Ali
Silima,miezi 5 uzito kilo 7.3 katika Hospitali ya Kivunge wagojwa wa
nje,baada ya kifungua Hospitali hiyo kwa niaba ya Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,jengo hilo limejengwa kwa ufadhili wa Shirika lisilo la kiserikali
(HIPZ) kutoka Uingereza,(katikati) Dkt.Tamim Hamad Said Daktari Dhamana
Hospitali ya Kivunge na Muuguzi Filonema Raumond Woga
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame kwa
niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali
Mohamed Shein,akifungua pazia kufungua Jengo la Wagonjwa wa Nje
Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini
Unguja,katika shamra shamra za Mapinduzi matukufu ya Zanzibar kutimia
miaka 52 (wa pili kushoto) Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo
Jecha
Wawakilishi
wa Mashirika ya Misaada ya kimaendeleo ambayo yamesaidia vifaa mbali
mbali wakitoa salamu zao wakati wa ufunguzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A.Unguja leo lililofunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame Mwadini ,kwa niaba ya Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame Mwadini akitoa hutuba ya ufunguzi waJengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A.Unguja leo kwa
niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali
Mohamed Shein, jengo lililojengwa kwa ufadhili wa shirika lisilo la
kiserikali la (HIPZ) kutoka nchini Uingereza ikiwa ni katika
shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar (kulia) Katibu Mkuu
wa Wizara ya Afya Dkt>Saleh Mohamed Jidawi na Naibu Waziri wa Afya
mahmoud Thabiti KomboJecha
Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo alipokuwa akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame Mwadini kutoa hutuba ya ufunguzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A.Unguja leo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na mashirika ya kimaendeleo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame Mwadini akitoa hutuba ya ufunguzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A.Unguja leo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame
Mwadini akipokea Kadi ya Mfuko wa Taifa wa Afya Kutoka kwa Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo Bw,Michael Mhando,kadi hiyo imetolewa kwa
ajili ya Mzee Makame Mjombo wa Gamba mweye umri wa miaka 140,wakati wa
sherehe za ufunguzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A.Unguja leolililofunguliwa kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na Ikulu, ZNZ
STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 9.1.2016
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein amesema kuwa hatua za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
Awamu ya Saba za kuimarisha huduma za afya za vijijini ni miongoni mwa
utekelezaji wa shabaha ya Mapinduzi ya mwaka 1964 ya kuzifikisha huduma bora za
afya hadi vijijini kwa nia ile ile ya waasisi wa Mapinduzi.
Dk. Shein aliyasema
hayo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais
Ikulu na Utawala Bora Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, mara baada ya kulifungua
jengo la wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Kivunge, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Katika hotuba hiyo,
Dk. Shein alisema kuwa huduma bora za
afya kwa wananchi wote bila ya ubaguzi ni miongoni mwa malengo ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 ambapo Chama cha ASP kilichoongoza Mapinduzi
hayo katika manifesto yake, kiliweka bayana azma yake ya kutoa huduma za afya
bure bila ya ubaguzi wakati kitakaposhika hatamu za Serikali.
Dk. Shein alisema kuwa
jitihada kubwa zimefanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kipindi
cha miaka 52 ya Mapinduzi katika kuimarisha huduma za afya kwa kutambua kwamba
afya bora ni muhimu kwa wananchi ili waweze kuishi vyema katika kazi ya kuleta
maendeleo ya nchi yao.
Alisema kuwa mafanikio
makubwa yamepatikana katika utekelezaji wa mipango na mikakati ya kuiendeleza
sekta ya afya nchini kupitia vitengo na programu mbali mbali zinazoendeleshwa
na Serikali kwa ushirkiano na Washirika wa Maendeleo.
“Nyote ni mashahidi wa
kuimarika kwa huduma za afya katika hospitali na vituo vytetu vyote va afya...
Aidha, kuna ongezeko kubwa la vituo vya afya vya daraja mbali mbali kiasi
kwamba hivi sasa wananchi wa Zanzibar hawawezi kwenda zaidi ya kilomita tano
bila ya kukuta kituo cha afya”,alisema Dk. Shein.
Akieleza historia ya
huduma za afya katika Mkoa wa Kaskani Unguja, Dk. Shein alisema kuwa kabla ya
Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 katika Mkoa huo kulikuwa na vituo viwili tu
vya afya ambavyo vilikuwepo huko Mkokotoni na Chaani.
Alisema kuwa katika
kipindi cha miaka 52 ya Mapinduzi Mkoa huo hivi sasa una vituo vya afya 26
ambapo vituo 18 ni vya daraja la kwanza na 7 ni vya daraja la pili pia, kuna
hospitali ya Koteji ya Kivunge ambayo lengo la Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Awamu ya Saba ni kuipandisha daraja kuwa hospitali ya Wilaya.
Dk. Shein alisema kuwa
lengo la mradi huo ulioanza mwaka 2012 ni kuziimarisha huduma za afya katika
hospitali zote za Koteji ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali
kuu ya Mnazi mmoja.
Aidha, Dk. Shein
alisema kuwa Serrikali imekusudia kuzisogeza huduma za afya kuwa karibu zaidi
na wananchi ikiwa ni pamoja na huduma za upasuaji kwa kinamama wajawazito,
huduma za uchunguzi kama vile za maabara, “X-ray” na “Ultra-sound”.
Pamoja na hayo, Dk.
Shein alitumia fursa hiyo kutoa shukurani za dhati kwa Shirika lisilokuwa la
Kiserikali la Uingereza HIPZ, UNICEF na ROTARY Club kwa kuiunga mkono Serikali
katika lengo la kuiimarisha hospitali hiyo.
Dk. Shein alisema kuwa
huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo zimeimarika sana baada ya Serikali
kupitia Wizara ya Afya kuongeza wafanyakazi, vifaa vya uchunguzi wa maradhi na
kuongeza aina za huduma zinzotolewa katika hospitali hiyo.
Sambamba na hayo, Dk.
Shein alitumia fursa hiyo kuwahimiza wazazi juu ya umuhimu wa kwenda
kujifungulia hospitali na kuhudhuria kliniki ili kupima na kupatiwa ushauri
pamoja na kuhakikisha watoto wanapelekwa vituoni kupatiwa chanjo kwa kuzingatia
kampeni ya chankji kwa watoto zinazoendeleshwa na Wizara ya Afya.
“Serikali itaendelea
kuzipatia ufumbuzi changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya afya kwa lengo
la kuwapatia huduma bora za afya wananchi wote mjini na vijijini”,alisema Dk.
Shein.
Aidha, Dk. Shein
alitoa wito kwa wananchi wote kuendelea kusherehekea maadhimisho ya miaka 52 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa amani na utulivu.
Nae Naibu Waziri wa
Wizara ya Afya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo aliwaeleza wananchi waliohudhuria
uzinduzi wa hopaitali hiyo kuwa hatua hizo ni miongoni mwa ahadi za Dk. Shein
kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambazo ameziahadi na sasa anaendelea
kuzitekeleza huku akitoa shukurani kwa washirika wa maendeleo yakiwemo Mashirika
ya Umoja wa Mataifa kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar.
Nae Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya Mohemmed Saleh Jidawi alisema kuwa juhudi mbali mbali zinaendelea kuchukuliwa na
Serikali chini ya uongozi wa Dk. Shein katika kuhakikisha Hospitali za Koteji
kuwa za Wilaya na kueleza kuwa gharama za ujenzi huo ni milioni 461 chini ya
ufadhili kutoka kwa Shirika la HIPZ.
Dk. Jidawi alisema
kuwa lengo ni kuhakikisha hospitali hiyo inakuwa ya Wilaya na kulipongeza
Shirika la HIPZ kwa kuendelea na juhudi zake katika kuiimarisha hospitali ya
Kivunge kama ilivyofanya kwa hospitali ya Makunduchi.
Alisema kuwa hospitali
hiyo ina uwezo wa kupokea wagonjwa 120 hadi 140 kwa siku mbapo pia hopsitali
hiyo itafanya kazi kwa masaa 24 huku akieleza kuwa hospitali hiyo inatumia
mfumo wa kisasa wa kuwaorodhosha wagonjwa kwa njia ya Kompyuta kwa lengo la
kupunguza kupotea kwa kumbukumbu.
Nao Washirika wa
Maendeleo wakiwemo wawakilishi wa HIPZ, UNICEF,ROTARY CLUB pamoja na uongozi wa
Mfuko Taifa wa Bima za Afya waliahidi kuendelea kuiunga mkono Serikali katika
kuiimarisha zaidi huduma za afya hapa nchini ikiwa ni pamoja na kukiendeleza
kituo hicho cha afya ili kitoehuduma bora kwa wananchi.
Aidha, washirika hao
walieleza kuwa kituo hicho kitakuwa ni mkombozi kwa akina mama na kutoa
shukurani kwa mashirikiano wanayoyapata kutoka kwa uongozi wa Wizara hiyo.
Viongozi mbali mbali
wa vyama na serikali pamoja na mamia ya
wananchi walijitokeza katika hafla hiyo.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment
paulmkale