Afisa
Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini
Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akitoa maelezo ya namna wanavyoendesha
shughuli zao kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla aliyefanya ziara ya kushtukiza
katika ofisi hizo, Januari 4, 2016. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Modewjiblog, Team.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi
Kigwangalla ameagiza watanzania wote wasikubali kutozwa rushwa kwa
ajili ya damu salama na baadala yake kwa mtu atakayefanya hivyo
watamchukulia hatua kali.
Kauli
hiyo imetolewa mapema Januari 4 (jana) na Naibu huyo wa Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Kingwangalla
alipofanya ziara katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo
jijini Dares Salaam.
Dk.
Kigwangalla amefafanua kuwa, kwa watu wote ikiwemo Nesi, Daktari ama
mtaalamu wa afya, atakayemtoza mtu damu, atachukuliwa hatua kali ikiwemo
kufukuzwa kazi.
“Kwa
watanzania wote, msikubali kutoa rushwa kwa ajili ya damu. Na kama
itatokea Nesi ama Daktari ama nani, anakuambia ulipie ili upate damu!.
Kwa sababu kuna uhaba wa damu kwa sasa.. Ripoti kwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu
wa Mkoa ama Daktari Mkuu husika ama fika Wizara ya afya moja kwa moja
na kuna namba tutaitoa kwa watanzania wote mtupatie ripoti.
Mtu
atakayekutoza damu, wewe tuambie, huyo tutamfukuza kazi moja kwa moja,
hatuwezi kuendekeza watu wa namna hii... Serikali inaingia gharama kubwa
kukusanya damu kwa watu, Kuna watu wanajitolea damu zao bure. Leo wewe
nesi ama mganga ukauze damu, hilo jambo hatutakubali hata kidogo kwa
hiyo natoa rai kwa watanzaia hiyo damu ni bure na haiuzwi na usikubali
kuuziwa damu hata kidogo.” Ameeleza hilo Dk. Kigwangalla.
Awali
katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla ameipongeza Ofisi ya Mpango wa Taifa
wa Damu Salama kwa kazi wanayofanya na ubunifu waliofikia wa kuhusisha
Halmshauri katika ukusanyaji wa damu huku wao wakisimamia kudhibiti
viwango vya damu ya matumizi kwa watanzania huku akitumia wasaha huo
kutoa maelekezo ya kuboresha mfumo wa motisha kwa wanaochangia damu
salama ambapo kwa wachangiaji damu kuingizwa kwenye mfumo wa
kieletroniki wa kuwatambua watu wanaochangia damu, kutoa taarifa jinsi
damu zao zilivyookoa miasha ya wagonjwa na kuwapa motisha ili waweze
kuwa wachangiaji endelevu.
“Motisha
sio soda na maji kwa wanaochangia damu. Motisha ni hata kupewa taarifa
kwamba damu yake imesaidia kuokoa maisha ya mwanadamu mwenzake aliyekuwa
anaumwa ugonjwa fulani, hii ni motisha kubwa sana kuliko hata pesa, ama
soda ama maji yanayotolewa anapochangia damu..
Lakini
kama imeshajitokeza mtu kuwa na tabia ya kuchangia damu, huyu sio wa
kumpoteza, maana yake kuna uwezekano mkubwa wa akarudi tena kuchangia
damu, mtu huyu ni lazima kuwe na mfumo wa kielekrioniki wa komputa wa
kumtakia salamu, taarifa na anakuwa kwenye database yenu.(P.T)
“Mnatakiwa muwe na mfumo wa kumpa taarifa pindi damu yake imetumika,
ikiwemo kumueleza kuwa damu yako imemsaidia Mama mjamzito aliyejifungua
na kutokwa damu nyingi, na mtu huyo akipata taarifa hiyo ni motisha
tosha hivyo ni lazima muwe na huo mfumo kutoa motisha zaidi.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi
Kingwangalla na msafara wake wakishuka ngazi kuelekea kukagua idara
mbalimbali katika ofisi hizo, Januari 4, 2016
Awali
akielezwa na Meneja wa kanda ya Mashariki katika Ofisi za Mpango wa
Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Eveline Mgassa
kwamba changamoto zilizopo katika upatikanaji wa damu nchini ni
halimshauri kutenga bajeti za kutosha kwa ajili ya huduma hiyo, Kwa
hatua hiyo, Dk. Kigwangalla ameziagiza Halmshauri zote nchini
kuhakikisha zinatenga bajeti za kutosha ilikusapoti mpango wa damu
salama.
Katika
hilo Dk. Kigwangalla ameapa kuwashughulikia wale wote watakaozembea na
kuwachukulia hatua kali Ma DMO, Wakurugenzi na kushtakiwa kwa mamlaka
zilizopo na kufukuzwa kazi.
“Naziagiza
Halmashauri zote kuhakikisha zinatenga bajeti za kusapoti mpango wa
ukusanyaji damu salama. Na Halmashauri zitakazoshindwa, DMO na
Mkurugenzi wake tutahakikisha tunawashtaki kwa mamlaka zilizowateua ili
uteuzi wao ukome mara moja. Maana hatuwezi kuacha akinamama wajawazito
wapoteze damu wakati wa kujifungua, watu wanaopata ajali wapoteze maisha
kwa sababu ya watu hawataki kutimiza wajibu wao.
Hilo
haliwezi kukubalika, Mfumo wa hali ya damu kwa Tanzania kwa sasa
unatisha. Kwa sasa nchi inakiwango cha chini mno, tokea wafadhili
wajiondoe katika hili. Ni lazima tuwe makini sana maana leo mzima kesho
umepata ajali, umepasuka mfupa wa kwenye paja damu nyingi zimemwagika
unahitaji damu!!
Kwa
upande wa watu wote wanaopata damu salama nchini, huduma hiyo wanazipata
bure kwani damu hizo ni za Serikali, Hata hivyo mifuko na vitu
vinavyotumika kuhifadhia damu hiyo vina gharama kubwa.
“Damu
inatolewa bure na serikali. Mtambue kuwa, vifaa vya kutunzia damu hii ni
gharama kubwa. Hivyo mifuko mashirika ya Bima, na mashirika mengine
kuanzia leo kutazama namna ya kulipa gharama za vifaa vya utunziaji damu
hizo. Damu ni bure, lakini mfuko ule wa kutunzia ile damu ni gharama
kubwa sana na hata vifaa vya kupimia damu ile nayo ni gharama kubwa
hivyo walipie kwa kila damu watakayochukua.” Alieleza Dk. Kigwangalla.
Meneja wa
kanda ya Mashariki Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo
jijini Dar es Salaam, Eveline Mgassa (mwenye miwani) akielezea utaratibu
wa ukusanyaji wa damu unavyofanyika kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla aliyefanya
ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo, Januari 4, 2016 jijini Dar.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi
Kingwangalla (aliyeipa mgongo kamera) akisikiliza maelezo kutoka kwa
Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo
jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma ya namna wanavyopokea watu
wanaofikia kuchangia damu kwa hiari na kuhifadhiwa kwenye benki hiyo
yaTaifa ya Damu Salama, alipofanya ziara ya kushtukiza, Januari 4, 2016
katika ofisi hizo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi
Kingwangalla akitoa mkono wa pongezi kwa wananchi walioonyesha uzalendo
kwa kufika katika ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Januari 4,
2016 na kuchangia damu kwa hiari yao ambapo mmoja kati yao alisema hii
ni mara yake ya nne na ni utararibu aliojiwekea.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi
Kingwangalla akisalimiana na kumpongeza mmoja wa wananchi (jina lake
halikuweza kupatikana) aliyefika kuchangia damu kwa hiari, Januari 4,
2016 katika makao makuu ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi
Kingwangalla akiwa ndani ya maabara ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama
alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi hizo, Januari 4, 2015 jijini
Dar es Salaam.
Afisa
Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini
Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akimwonyesha Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla
moja ya damu ambayo ni maalum kwa wamama wajawazito wakati wa kujifungua
zilizohifadhiwa kwenye jokofu katika mabara hiyo.
Mmoja wa
watumishi katika maabara ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama
(ambaye jina lake halipatikana) akiendelea kutekeleza majukumu yake kama
alivyokutwa na mpiga picha wetu.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi
Kingwangalla akisaini vitabu vya wageni nje ya ofisi za Mpango wa Taifa
wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Januari 4, 2016 wakati
alipofanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya ziara ya kushtukiza na kuzungikia vitengo mbalimbali katika ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
paulmkale