WEMA
Sepetu ‘Madam’ ni mashine ya kutafuna fedha! Ndivyo unavyoweza kusema
kufuatia habari za mjini kumtaja staa huyo wa Bongo Movies kuwa
ameteketeza takriban Sh. Mil. 300 za mbunge ambaye anadaiwa kuwa ndiye
anayemweka mjini kwa sasa, Risasi Mchanganyiko limenasa ubuyu kamili.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Wema
na mbunge huyo (jina kapuni kwa sasa) wanadaiwa kuwa walianzisha
uhusiano wa kimapenzi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika
Oktoba 25, mwaka jana ambao matokeo yake yalimpa ushindi Dk. John Pombe
Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Rais wa Awamu ya Tano ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Inadaiwa uhusiano huo tayari umezaa
matunda kwani mlimbwende huyo ni mjamzito.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa
mujibu wa chanzo makini, mara baada ya mrembo huyo asiyechuja Bongo
kuwa ‘klozi’ na mbunge huyo kijana mwenye pesa ndefu katika kampeni hadi
sasa, amemchuna mbunge huyo kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya matumizi
na zawadi mbalimbali alizomnunulia.
RANGE MIL 200
“Mbunge
alimpa ahadi tu akimaliza kampeni anampa zawadi ya Range Rover yenye
thamani ya shilingi milioni 200, ilikuwa maalum kwa ajili ya bethidei
yake maana hakuweza kufanya sherehe hiyo iliyomuangukia akiwa kwenye
kampeni. Alipomaliza tu, mtoto wa kike akapewa ndinga yake japo alificha
kwa kusema amejizawadia mwenyewe.
SHOPPING USIPIME!
“Yaani
Wema akiwa ndani ya kampeni alikuwa halali hoteli za kimaskini, hizo
shopping ndiyo usiseme. Kipindi kile cha kampeni shopping moja tu ya
viatu, cheni, gauni na mazagazaga mengine ilikuwa si chini ya milioni
mbili au tatu hivi. Kafanya nyingi tu za aina hiyo.
“Sasa achana
na hizo, kwenye sherehe za Krismasi, Boxing Day na Mwaka Mpya nasikia
katekeketeza milioni 25 kwa mavazi na mazagamazaga aliyopika kula yeye
na marafiki zake wa karibu pamoja na ndugu zake, mbunge kasimamia shoo
bila wasiwasi wowote,” kilisema chanzo hicho.
KUKAA HOTELI DAR
Chanzo
hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, baada ya kumaliza kampeni, Wema
alirejea jijini Dar lakini kutokana na hali yake alimwambia mbunge
amlipie hoteli kwani hakujisikia kuendelea kuishi pale Kijitonyama
alipokuwa anaishi.
ATEKETEZA MIL. 40
“Yaani huwezi amini pale
hotelini (jina lipo) aliteketeza kitu kama shilingi milioni 40 hivi kwa
kupanga na kula kwa zaidi ya siku 15. Mbunge hapo alikunjuka tu bila
wasi maana fedha kwake si tatizo.
NYUMBA MIL. 12
“Baada ya
kuona mmiliki wa nyumba ya Kijitonyama amemtaka Wema kuhama katika
nyumba yake, kigogo akaona isiwe tabu, akampangia nyumba nyingine kali
zaidi maeneo ya Ununio jijini Dar kwa shilingi milioni 12 kwa mwaka
mzima.
MISELE YA MAFUTA, STAREHE MIL. 23
“Wema muoneni
hivihivi tu, mtu wake anayemsimamia kaniambia kwa kuweka mafuta kwenye
gari, tangu mwezi wa 11 mwaka jana alipoanza kulitumia lile Range,
kateketeza shilingi milioni na kama haitoshi, ametumia shilingi milioni
13 kwa ajili ya mitoko ya usiku kuwapa watu watunze na yeye kutunza
wanamuziki mbalimbali katika bendi ukijumlisha na vinywaji na vyakula,”
kiliweka nukta chanzo hicho.
NI REKODI YA AINA YAKE
Akizungumzia
matumizi hayo ya fedha, mmoja wa mastaa wakubwa ambaye aliomba hifadhi
ya jina, alisema kwa matumizi hayo makubwa aliyoyafanya Wema ndani ya
miezi kadhaa ni dhahiri kwamba ndiye staa wa kwanza wa kike kutumia
fedha nyingi ndani ya muda mfupi.
“Wewe fikiria tunasikia kina
Lulu, Kajala na wengineo wamepangiwa nyumba lakini husikii kama kuna
gharama nyingine kubwa kama Range, mafuta, shopping, kupanga hoteli
ambazo kwa ujumla wake zinafikia shilingi milioni 300,” alisema staa
huyo.
MBUNGE ASAKWA
Jitihada za kumpata mbunge huyo machachari
aliyekuwa akitema cheche mara kwa mara kwa viongozi wa vyama vya
upinzani, hazikuzaa matunda lakini rafiki yake wa karibu alikiri kuwa
mbunge huyo amemwaga fedha nyingi kwa Wema.
“Daah jamaa (mbunge)
kafa kaoza hizo milioni 300 mbona kidogo ni zaidi ya hizo, wewe
unafikiri tangu kipindi cha kampeni hadi leo na matumizi ya Wema
yanayohusisha na wapambe wake ni mchezo?” alisema rafiki huyo.
WEMA ANASEMAJE?
Alipotafutwa Wema ili kuzungumzia matanuzi hayo simu yake iliita bila kupokelewa licha ya kutumiwa ujumbe mfupi, bado hakujibu.
No comments:
Post a Comment
paulmkale