New Video: Harmonize Ft.Diamond Platnumz - Bado (Official Video)
Mabibi na mabwana, Harmonize ft Diamond Platnumz wamekusogezea hii ya ‘Bado’| Download MP4
Cooming Soon New Song: Diamond Platinumz - #Simba
Diamond kuachia wimbo wa kurap uitwao ‘Simba’Staa wa muziki Diamond Platnumz amejipanga kuachia wimbo mpya wa kurap uitwao Simba. Akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa hii, Meneja wa msanii huyo, Babu Tale alisema wimbo huo utakuwa sio wa biashara bali ni zawadi kwa mashabiki. “Kama Hip Hop ni biashara Diamond amefanya wimbo wa kurap lakini hatujauchulia kama ile biashara.Wimbo umeshaisha bado tu kuuachia,kwa hiyo mashabiki wangu wakae mkao wa kula.
Yanga yasonga mbele klabu bingwa Afrika
Mabingwa
wa soka Tanzania Bara na wawakilishi katika michuano ya Ligi ya
Mabingwa Afrika, Yanga SC leo imefanikiwa kuitoa Cercle de Joachim ya
Mauritius kwa jumla ya mabao 3-0, kufuatia ushindi wa 2-0 jioni ya leo
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo wa kwanza ilishinda bao 1-0.
Alikuwa
ni Amissi Joselyn Tambwe, mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi ambaye
aliifungia Yanga bao la kwanza katika dakika ya tatu ya mchezo kwa
kichwa akimalizia kwa uzuri krosi ya winga Simon Msuva.
Yanga
waliendelea kulishambuliwa lango la wapinzani wao lakini kukosekana kwa
umakini wa washambuliji wao kuliwanyima magoli mengi zaidi.
Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Yanga walikuwa na akiba ya bao 1-0.
Kipindi
cha pili Yanga waliingia na nguvu mpya na kufanikiwa kuongeza bao la
pili lililofunga na Thaban Scara Kamusoko mnamo dakika ya 56 kwa shuti
kali akiwa nje ya boksi, baada ya kuanzishiwa mpira wa adhabu na beki
Mwinyi Hajji Mngwali.
Kwa
matokeo haya Yanga sasa itakutana na APR kutoka nchini Rwanda baada ya
kuwatoa Mbabane Swallows ya Swaziland kwa jumla ya mabao 4-2 katika
Raundi ya Pili.
Yanga:
Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Kevin Yondani,
Vincent Bossou, Mbuyu Twite/Pato Ngonyani dk46, Simon Msuva, Thabani
Kamusoko, Amissi Tambwe, Malimi Busungu/Paul Nonga dk46 na Deus
Kaseke/Godfrey Mwashiuya dk76.
Cercle
de Joachim: Abrefa Godfrey Yaw, Buckland Jimmy Hendrick/ Laretif Stan
dk83, Balisson Paschal Damien, Natrey Isaac, Bazerque Desire, Permal
Cedric, Langue Jean Anderson, Rasdarising Bhavish/Maguy Jacque Daniel
dk78, Pithiaj Louis Fabien, Odame Abraham na Chiffone Louis Guiyano
Baada ya Rich Mavoko Kukana Kutoka Kimapenzi na Gigy Money, Gigy Aanika Chat zao
Gigy Money, alipost instagram chat hizo na kila moja kuiandika ujumbe wake. Hata hivyo baade alizifuta post hizo.
“Mimi mwenyewe sikujui vilevile” aliandika Gigy.
“Ahahhahaha unajua mavoko ntakudhalilishaaa ….mm ni mkimyaaa tu sio Mpole ata kidogo …unajikuta umenisahau bwege ww” aliandika Gigy.
“Banduguuuuuu kujichubua kwako ndio nkuogope weeee Richard wewe umeombaaa watu wanipigie nisikutie aibu sasa unaletaaa utoto sina nachokipoteza kumbukaaa I don’t care��������” aliandika Gigy
Subscribe to:
Posts (Atom)