Imefahamika kuwa mshambuliaji tegemeo wa Lipuli FC, Adam Salamba, atapokea mshahara wa shilingi milioni mbili kwa kipindi cha miaka miwili ambacho ataichezea Simba, ambao ni sawa na shilingi milioni 48 kwa mkataba wake wote.
Mshambuliaji huyo alisaini mkataba huo wa miaka miwili juzi akitokea Lipuli ambayo ilimuuza baada ya Yanga na Azam FC kushindwa kuinasa saini ya nyota huyo wa kupachika mabao.
Salamba aliyemaliza msimu na mabao sita, anatarajia kuungana na mshambuliaji wa Majimaji FC ya Ruvuma, Marcel Boniventure aliyefunga mabao 14 kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Bara.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata gazeti la Championi, Salamba alisaini mkataba huo wa miaka miwili kwa dau la shilingi milioni 40.
Mtoa taarifa huyo alisema, katika dau hilo la usajili lililotolewa na Simba, shilingi milioni 25 zilikwenda kwa timu yake ya zamani ya Lipuli, iliyommiliki kwa ajili ya kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja wa kuendelea kuichezea timu hiyo.
“Uongozi wa Lipuli ni lazima unufaike na mauzo ya Salamba, kama unavyofahamu mchezaji alikuwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuichezea Lipuli.
“Hivyo, kabla ya mchezaji huyo kusaini mkataba, yalifanyika mazungumzo kati ya sisi timu tunaommiliki mchezaji, mchezaji mwenyewe na uongozi wa Lipuli kwa ajili ya kukubaliana baadhi ya vitu ikiwemo kupata sehemu ya fedha kwa ajili ya kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja katika dau hilo la usajili.
“Uzuri ni kwamba hayo yote yalifanyika na kufikia muafaka kuwa sisi Lipuli tupatiwe shilingi milioni 25 za kusitisha mkataba wa Salamba pamoja na makubaliano mengine ya binafsi kati ya mchezaji na uongozi wa Simba.
No comments:
Post a Comment
paulmkale