Licha ya kumaliza msimu kwenye nafasi ya tatu ambayo ni mbaya zaidi kuwahi kuwatokea katika miaka ya hivi karibuni, Yanga imekumbana na kasheshe jingine ambalo limefanya mambo yao kuwa mabaya zaidi.
Simba na Azam zimeamua kuanzia vurugu zake za usajili katika kikosi cha Yanga ambapo zote mbili zimeikomalia kwelikweli huku mastaa wakubwa wa Jangwani wakionekana kupagawa na mafungu waliyowekewa mezani.
Usajili rasmi unaanza Juni 15 lakini Simba na Azam zimeanza kuvuna Jangwani. Kwanza Yanga walikuwa wanamtaka Adam Salamba kutoka Lipuli, lakini juzi jioni aliwashangaza wengi baada ya kutua Simba kwa kile kilichodaiwa kuwa Yanga walishindwa kufikia dau linalotakiwa.
Simba wamempa Salamba Sh40milioni taslimu na jana Jumanne walimkabidhi gari ya kutembelea aina ya Crown mpya yenye thamani ya zaidi ya Sh15milioni.
Kwa mujibu wa gazeti la Championi, limeeleza kuwa linafahamu kuwa wachezaji muhimu wa Yanga wanaondoka na kujiunga Azam na Simba na kilichobaki ni ishu ya muda tu kwani wameshashawishika.
Wachezaji wanaotarajiwa kuondoka ni Papy Kabamba Tshishimbi, Kelvin Yondani, Hassan Kessy na Obrey Chirwa huku Donald Ngoma yeye akiwa ameshasaini Azam, kila mmoja ataondoka kwa dau lake na sababu kubwa ni ukata na maisha magumu ndani ya Yanga ambapo hawapati sapoti yoyote kwa wadau kama awali.
Lakini nje ya Yanga Simba wanaweza kuwanasa pia, Pascal Wawa na Tafadzwa Kutinyu kutoka Singida United.
PAPY TSHISHIMBI:
Huyu bado ana mkataba wa mwaka mmoja kwa sasa, lakini Simba wamepania wanamtaka na wana nia kweli, muda wowote unaweza kusikia chochote.
“Huwezi kuamini hata y e y e mwenyewe a n a t o a ushirikiano m k u b w a kwa Simba na hata l e o ( j a n a ) tutawasiliana nae tena,”alisisitiza kiongozi mmoja makini wa Simba.
“Huyu Simba wanaweza kuwapa Yanga hata milioni 100,hela ipo sasahivi, Yanga wanatafuta hela ya kusajili,”kiliongeza chanzo chetu cha uhakika.
Hata hivyo, imefahamika kuwa mchezaji huyo naye anataka kuondoka kwenye timu hiyo kutokana na hali ya kiuchumi kuwa mbaya hivyo anaweza kuwashawishi viongozi wake wakavunja mkataba na kujiunga na timu hiyo.
Tshishimbi alisaini mkataba wa miaka miwili na sasa amebakiza mwaka mmoja tu na kuna baadhi ya vitu kwenye mkataba wake ambavyo inaelezwa Yanga hawajavitimiza ambavyo vinaweza kumruhusu akauvunja mkataba huo.
KELVIN YONDANI
Awali ilikuwa inaelezwa kuwa Simba wanamtaka beki huyo lakini kibao kimebadilika na sasa anaweza kwenda kujiunga na Azam.
A n a y e t a r a j i w a kuwa kocha mpya w a A z a m kuanzia msimu ujao, Hans van Pluijm amepende k e z a jina la beki huyo m w e n y e uwezo wa juu kuwa asajiliwe na timu hiyo.
H a t a hivyo, hakuna kizuizi chochote kinachomzuia kwenda kwenye timu hiyo kwa kuwa hadi sasa yeye ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika.
HASSAN KESSY
Hakuna aliyekuwa a n a f i k i r i k u h u s u H a s s a n K e s s y k w e n d a A z am, l a k i n i m a m bo yanaelezwa kuwa y a m e b a d i l i k a baada ya beki aliyekuwa anatakiwa na timu hiyo Juma Abdul kugoma kuondoka Yanga, ndiyo wakaweka nguvu kwa Kessy ambaye naye h a n a mk a t a ba na timu hiyo ya Jangwani.
Kessy anawadai Yanga na wala hajasaini mkataba hadi sasa, Azam wameshazungumza naye na kuna uwezekano mkubwa akasaini wiki hii kwa kuwa kila kitu kinaonekana kuwa tayari kukamilika alisema mtu wa karibu na Kessy.
PASCAL WAWA
Kwa mashabiki wa soka la Tanzania wanamfahamu beki huyo kisiki raia wa Ivory Coast, lakini habari ya kushtua ni k w a m b a a n a k u j a nchini na k u s a i n i S i m b a mwaka mmoja.
Simba wanamtaka Wawa kwa kuwa wanafahamu kuwa ana uzoefu wa kimataifa na atawasaidia sana msimu ujao ambao wanaingia kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
Wawa amemalizana na timu yake ya sasa El Merreikh ya Sudan na ameshafanya mazungumzo ya awali na kiongozi mmoja wa Simba na inaelezwa katika mazungumzo yao mchezaji huyo amesema anahitaji mshahara tu kwanza apige kazi bila fedha yoyote ya usajili.
Inaelezwa kuwa akiwa Sudan alikuwa anaendelea kuwa mchezaji tegemeo kama wakati akiwa na Azam.
TAFADZWA KUTINYU
Habari nyingine njema kwa mashabiki wa Azam, ni kwamba klabu yao imepindua meza na tayari imekamilisha usajili wa kiungo wa Singida United, Mzimbambwe Tafadzwa Kutinyu.
Awali uongozi wa Singida ulionekana kuweka ngumu mchezaji huyo kujiunga na Azam lakini mwenyewe alishinikiza kuwa anataka kuondoka na kwenda Azam.
Kocha Pluijm alishindwa kumshawishi kuendelea na timu ya Singida kwa kuwa timu hiyo inashiriki michuano ya kimataifa na hivyo akasema anakwenda Azam lakini kwa mzuka wa viongozi wa Azam walionao lolote linaweza kutokea.
Siyo kimataifa tu hata fedha kwa kuwa ingekuwa ni hivyo angesubiri Singida wacheze na Mtibwa fainali ya Kombe la FA kwani wangeweza kupata nafasi hiyo lakini yeye alisisitiza kuwa anataka kwenda Azam na inasemekana amesajiliwa Azam kwa gharama ya dola 20 , kilisema chanzo kutoka Singida.
OBREY CHIRWA
S i m b a w a m e shasema k u p i t i a msemaji wao Haji Manara kuwa watakwenda nchini Kenya kwenye michuano ya SportPesa na jina kubwa kwenye mic h u a n o hiyo zaidi ya Salamba na taarifa zinasema kuwa wapo karibu sana kumalizana na Chirwa ambaye mambo yake yanasimamiwa na Jonas Tiboroha.
Habari zinasema kwamba Chirwa anataka kutua Msimbazi na ana nafasi kubwa ya kumrithi Laudit Mavugo ambae bado yupo Sinza, Dar es Salaam anakula bata lakini ameshapigwa chini.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa kuna vita kubwa sana kati ya Simba na Azam kuhusu mchezaji huyo.
Ofisa Habari wa Simba alisisitiza jana Jumanne kwamba; “Tutalipiza kila aina ya kisasi walichotufanyia wakati ule. Kwenye usajili tunafuata maelekezo ya Kocha lakini kuna sehemu fulani siasa za usajili zinaruhusiwa, unachomeka kidogo kumuumiza mtani wako.”
“Nakwambia tutashtua, kuna jina moja kubwa tunakwenda nalo Nairobi. Nakwambia tutashtua. Hao ambao mmeshawasikia mpaka sasa ni chamtoto,”alisisitiza Manara ambaye amekuwa ni mtu mwenye furaha kwa madai kwamba Yanga iliwazingua sana enzi za Mwenyekiti Yusuf Manji.
CHANZO: CHAMPIONI
No comments:
Post a Comment
paulmkale