Leo Jumatatu Juni 4 2018, klabu ya Azam inatarajia kumtangaza mchezaji mpya atakayesaini mktaba na klabu hiyo.
Mchezaji
huyo anatajwa kuwa ni kitasa cha kulia cha klabu ya Yanga Juma Abdul
ambapo utakuwa ni mwendelezo wa kusajili wachezaji kutoka kwenye klabu
hiyo ambayo imekaa kimya kuhusu suala la usajili.
Jaffar Maganga , Ofisa wa Habari wa Azam amueleza mwandishi habari hizi kuwa Jumatatu itakuwa siku maalumu ya kulipua bomu jingine.
Endapo
Abdul atatangazwa leo na Azam FC, atakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa
na Azam ndani ya mwaka huu baada ya Mzimambwe, Donald Ngoma.
No comments:
Post a Comment
paulmkale