Rich Mavoko wa WCB Wasafi abwagwa : Lulu Diva Adaiwa Kufaidi Penzi La Bill Nas

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Ona’ Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva amesemekana kuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzake Bill Nas.

Global Publishers wanaripoti kuwa wasanii hao wawili wamekuwa na ukaribu wa ajabu na wameonekana wakionyeshana Mahaba hadharani bila kujali macho ya watu.

Gazeti hilo linaripoti kuwa lilimpata mtu ambaye alitoa taarifa hiyo ambapo alifunguka:

Walianza kama masihara, tukajua labda Rich Mavoko ndiyo anakaa kwa Lulu kumbe ni Bill Nas bwana, juzi walikuwa tena pamoja wakielekea mkoani sijui mkoa gani lakini picha zao za kujibebisha zinamaanisha“.

Baada ya Tetesi hizo na kusindikizwa na picha kadhaa Kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha ukaribu Global Publishers lilimsaka Lulu Diva ambaye alimwaga povu hili:

Hivi jamani mtu kuongozana na mwanaume ndiyo kutembea naye? Mbona mnataka kuniharibia kwa mtu wangu niliyekuwa naye?
“Bill Nas ni mshikaji   wangu wa kawaida tu, juzi (Jumamosi iliyopita) tuliandaliwa shoo ya pamoja huko Iringa, tukiwa njiani tulikuwa tukipiga mapicha picha kama mtu na rafiki yake, nashangaa watu wanageu-zageuza maneno”.

No comments:

Post a Comment

paulmkale