Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) limetangaza kuufungia wimbo mpya wa mwanamuziki Rayvanny kwa maelezo kuwa unahamasisha masuala yasiyokubalika katika jamii.
Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza amesema kuwa wameufungia wimbo huo ambao amemshirikisha Diamond Platnumz na kupiga marufuku kuchezwa mahali popote.
Ameongeza kuwa wanawasiliana na mamlaka nyingine ili kuchukua hatua zaidi kwa kuwa tayari wimbo umeenea mitandaoni.
Kuhusu kupigwa katika tamasha lao la Wasafi linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 24 mwaka huu amesema nalo watalifungia iwapo watautumia.
Ameainisha kuwa maneno yaliyotumika katika wimbo huo yanahamasisha ngono kinyume na maumbile na matusi mengine yanayobomoa maadili.
No comments:
Post a Comment
paulmkale