Showing posts with label Chris Brown. Show all posts
Showing posts with label Chris Brown. Show all posts

Hamissa Mobetto na Ray C Ndani ya Bifu Zito

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amejikuta katikati ya bifu zito na mzazi mwenza wa Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto.

Sintofahamu hiyo Ilianza siku mbili nyuma baada ya Ray C kuzisema nguo aina ya ‘Fendi’ ni feki ambazo zimekuwa zikiuzwa sana na Hamisa ambaye ni mfanyabiashara ambapo Ray C alitoa kama maneno ya kejeli kuhusu nguo hizo ingawa hakutaja jina.
Basi Hamisa baada ya kuona kama Dongo lile katupiwa yeye basi moja kwa moja akaandika ujumbe ambao uliwakosoa watu ambao hawaonyeshi sapoti kwa biashara za wengine badala yake wanakuwa na wivu.
Baada ya sakata hilo na mashabiki wa Hamisa kumvamia Ray C basi aliweka wazi kuwa hakumtaja Hamisa jina kwa lile Dongo lakini baada ya kuona wanazidi ikabidi amvae Hamisa na kumsema kuhusu Zari na kudai yeye mwenyewe alimuumiza Zari kwa kitendo cha kuzaa na Diamond.
==

Collabo ya Diamond Platnumz Ft. Chris Brown inakuja, MTV Base Afrika Wamethibitisha

Kurasa iliyothibitisha na Instagram ya kituo cha MTV Base Afrika imethibitisha kuwa msanii wa kimataifa kutoka Tanzania Diamond Platnumz anafanya collabo na Chris Brown.

Diamond Platnumz ni miongoni mwa wasanii wakubwa Afrika aliyewahi kushinda tuzo za#MTVMAMA2015 #BESTLIVEACT #AFRIMMA2015  #AfricanArtistOfTheYear #AFRIMA2015 #AfricanArtistOfTheYear #MTVEMA2015 #BestAfricanAct na #BestWorldWideAct, Pia tuzo kama #MTVEMA.

Ukiacha Chris Brown, Diamond Platnumz ameshafanya collabo na Msanii kutoka Marekani Ne-yo.

Sio Joti pekee mwenye style mpya ya Nywele, mcheki Chris Brown.

209x132xAmazing-Chris-Brown-Blonde-Hair.jpg.pagespeed.ic.XPMzcJvpyy

Jana tulikuletea story kuhusu mtindo mpya wa nyewele wa Joti ambao uko tofauti kabisa na nywele zake zilivyowahi kuwa hapo nyuma .

Joti si star pekee aliyeanza mwaka 2015 akiwa na style mpya ya nywele , mkali wa miondoko ya R&B Chris Brown naye ameamua kuja na style ya tofauti ya nywele ambayo hajawahi kuwa nayo.

Style Mpya ya Nywele ya Chris Brown inaonekana hivi .

Style Mpya ya Nywele ya Chris Brown inaonekana hivi .

Chris Breezy ameamua kusokota rasta ndogo ndogo na kuachana na ile style yake iliyozoeleka ya kunyia nyewele fupi ya Lowcut ambayo kila mmoja ameizoea .

chris-brown-dreads

Hapo awali Brown aliwahi kuwa na style ya kuweka rangi ya dhahabu au blonde style ambayo ilimfanya aonekane tofauti na mwanzoni wakati nywele zake zilipokuwa fupi na nyeusi.

Awali Chris Brown alikuwa anapaka nywele zake rangi kama hivi .

Awali Chris Brown alikuwa anapaka nywele zake rangi kama hivi .

Kabla ya kuwa anapaka rangi nywele zake zilikuwa hivi .

 

Mwanzoni wakati anatoka Chris Brown alikuwa na nywele za chini 'Lowcut' .

Mwanzoni wakati anatoka Chris Brown alikuwa na nywele za chini ‘Lowcut’ .

 

Kabla ya kuwa anapaka rangi nywele zake zilikuwa hivi .