Ambwene Yessaya aka AY anatarajia kuachia ngoma mpya hivi karibuni, lakini safari hii wimbo anaoachia ni collabo aliyoshirikisha wasanii wa kimataifa.‘It’s Going Down’ ndio jina la wimbo huo ambao kawashirikisha Ms Triniti pamoja na
Lamyia wa Marekani.
Hii si mara ya kwanza kwa AY kufanya kazi na waimbaji hao wa kike, aliwahi kumsirikisha Ms Triniti kwenye wimbo wake unaoitwa ‘Good Boy’ uliotoka 2010, na Lamyia katika wimbo unaoitwa ‘Speak With Your Body’ wakiwa na Romeo.
Huu ni wimbo ambao umetayarishwa na producer wa kimataifa aitwaye Riley chini ya management ya Network Showbiz ya Marekani ambayo pia inamsimamia AY.
Wasanii wengine ambao wako chini ya Network Showbiz ni pamoja na Triniti, Lamyia, Alpha Rwirangira, Halima Namakula na Racheal.K. Tembelea website Network Showbiz hapa.
No comments:
Post a Comment
paulmkale