Tasnia ya Muziki Tanzania ilipata sura mpya na mtazamo mpya tangu
kipindi cha miaka ya 2000 pale tulipoona watu kama Mr. Ebbo, Professa
Jay, Juma Nature, Daz Nundaz na wengineo wakianza kuimba nyimbo zenye
Mrengo wa kiharakati zaidi na kukubalika za jamii kwa upana zaidi.
Lakini hakuna waliotikisa anga za muziki kwa nyimbo zenye Ujumbe mzito
na Ushawishi wa Kiwanaharakati na kisiasa kama hawa Wawili, nao ni John
Evans Simba (Dakta John) na Fredrick Gerson Mariki (Mkoloni) au kama
wengi tunavyowafahamu kama WAGOSI WA KAYA.
Kwanza kabisa, Wagosi
Wa Kaya walianza kwa kubadili aina ya Ujumbe uliokuwa unapatikana
kwenye muziki wa kizazi kipya, kwa kuongelea mambo ya kila siku
yanayosumbua jamii bila kuweka kificho cha aina yoyote. Pili ni aina ya
lugha na lafudhi waliyotumia, ambapo matumizi ya Lafudhi ya Kidigo na
Kisambaa. Hilo na kuchanganya na lugha ya ucheshi ya kufikisha ujumbe,
vilimfanya msikilizaji kuupokea ujumbe ilihali akiwa anaburudika.
Dkt
John na Mkoloni wana historia ndefu na Tanga, John alikulia akikata
Mashamba ya Mkonge na kupata elimu ya msingi ilihali akiendelea
kupambana na changamoto za kimaisha katika familia yao. Alishawahi
kunukuliwa akisema kuwa aliwahi kufanya kazi kwa kukodishwa, yaani
wanachukuliwa na mtu kwenda kufanya kazi kwenye mashamba, na hatimae
aliewapeleka alilipwa na yeye kuwalipa vibarua ujira wao huku akibaki na
sehemu ingine kama faida yake. Kwa upande wa Mkoloni, ingawa sehemu
kubwa ya familia yake, hasa wazazi wakiwa Jijini, yeye alikulia Tanga
ambako jamii yao ilikua ina tawi pia. Elimu pia alipatia mkoani Tanga
katika shule ya Popatlal.
Kuingia katika sanaa, Kuibuka kwa kundi
hili katika sanaa za muziki kulianza na mapenzi ya dhati waliyokuwa
nayo kwenye fani. John alianza kama Densa na mara nyingi alijiweka
katikati ya shughuli na kutoa burudani kutipia ufundi wake wa “Kubreak
Dance”. Ni Baada ya kukutana na Fredrick aliekuwa na kundi la Tanga
Line, na wengi mtamkumbuka Dani Msimamo ambae pia ni mmoja kati ya
vinara wa kundi hilo. Baada ya hao wawili kubadilisha mistari iliyokuja
kuzaa tungo ya “TANGA KUNANI” ndipo wakaona ipo haja ya kutoka kama
kundi na kufanya kazi pamoja kama Wagosi wa Kaya. Kuibuka kwa kundi hili
sio tu kulisaidia kuiweka Tanga katika Ramani ya Muziki wa Tanzania na
Afrika Mashariki, lakini pia kulisiaidia kwa kiasi kikubwa kuibua ukweli
juu ya Mji huu Mkongwe ambao hapo awali uliwahi kuvuma kama Kitovu cha
Biashara, Kilimo, Viwanda na Uchukuzi.
Katika kipindi chao kama
kundi, Wagosi walipata mafanikio makubwa sana wakiwan chini ya muandaaji
muziki Profesa Ludigo na Studio za MJ, na moja kati ya vibao
vilivyowapa umaarufu sana ni pamoja na TANGA KUNANI, WAUGUZI, TRAFIKI.
Hivi karibuni baada ya kupotea kwa muda, wamejiunga tena na kurudi
wakiwa wanaandaa tungo kadhaa za kuwarejesha tena kwenye ramani. Ingawa
wanakiri kuwa kurejea baada ya kuwa nje ya “game” kwa muda mrefu ni
kazi, kwani kuna wale waliokuwepo nao wakaendelea kuwepo, na kuna wengi
wapya walioibuka kwa kasi ya juu na bado wapo juu. Mnamo April mwaka
2014 waliachia Video mbili mpya za nyimbo za “Bao” na “Gahawa”, na
wanaahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii kuendelea kuwaburudisha
mashabiki wao wa zamani na wapya.
Katika Mkasi TV, tulipata fursa
ya kuzungumza nao, Salama, Mubarak na John waliweza kuhoji mengi zaidi.
Sikia na kutazama toleo hili kamili la video hapa hapa.
FURAHIA
L . O . V . E
Follow MkasiTV on
Facebook : http://facebook.com/MkasiTV
Twitter : @MkasiTV

No comments:
Post a Comment
paulmkale