Nomaa!!Mkali Wa Mavela Walter Chilambo Adai Kuwa Muziki Umekua Mgumu
Msanii wa muziki na mshindi wa shindano la Bongo Star Search, Walter Chilambo amesema anakutana na wakati mgumu kwenye muziki.
Walter amesema kuwa kwa sasa anajisimamia mwenyewe katika
kila kitu hali inayomfanya ashindwe kufanya vitu vyake kwa wakati.
“Unajua sasa hivi kuna changamoto kubwa kwahiyo kuna wakati mgumu,
mara huyu kafanya hiki mara huyu kaibuka. Pia kuna watu wanapeana stress
lakini mtu inabidi u-stick kwenye upande wako,” amesema msanii huyo.
“Ndio maana unakuta mimi na stick kwenye upande wangu na watu wangu pia,
najaribu kufanya kile kitu ambacho mimi nakiweza. Siwezi kujikuna
sehemu ambayo mkono haufiki, kwahiyo japo tunaenda tunarudi mimi naoga
game iko poa tu. Mimi sasa hivi niko mwenyewe sina management, sina
usimamizi wowote, kwahiyo inakuwa ni ngumu sana huwezi fanya kila kitu
peke yako inakuwa inanipa wakati mgumu sana. Kuna vitu vingine nahitaji
msaada kwa sababu peke yangu nakuwa siwezi. Kwahiyo hiyo ni kitu ambayo
inanisumbua, unakuta sometime vitu haviendi on time,” aliongeza.
Kwa upande mwingine Walter amezungumzia ujio wa video zake mbili mpya
baada ya ukimya katika muziki wake ambao anadai ukimya huyo ulitokana
na matamasha mbalimbali yanayoendelea hapa nchini.{Twitter@paulmkale/FB paul e kilas/Instagram paulmkale/Wathssap 0767527986}
“Yaani nitatoa video mbili, kuna moja ya wimbo wangu uliotoka, kuna
mwingine mpya kabisa. Hizi video hazitatoka kwa wakati mmoja zitatoka
kwa wakati tofauti tofauti lakini hazitapishana, unajua nataka nifanye
mashambulizi baada ya ukimya fulani.”
No comments:
Post a Comment
paulmkale