Kaa Tayari;Godzilla Kuja Na Ngoma Mpya"‘Illumi Naughty’Hapo Kesho
Rapper Godzilla anatarajia kuachia wimbo wake mpya uitwao ‘Illumi
Naughty’ kesho, wimbo ambao amedai kuwa video yake itatisha kwasababu
itakuwa na ishara za kishetani.
Godzilla amewataka watu wasiogope kwani anachohitaji ni kufikisha ujumbe wake kwa jamiii.
“Unajua kuna wazazi ukiwapelekea mke unakuta yale mavazi ya vimini,
kujipodoa, watakwambia mbona umetuletea shetani nyumbani, lakini unakuta
mapenzi hayaangalii mtu yukoje wala jinsi alivyo, kwahiyo wao wazazi
wanamwita shetani lakini siyo shetani. Sema wimbo siyo illuminati,
iluminati inawakilisha shetani, lakini naughty siyo shetani, kwaiyo
mzazi anaweza akamuona demu wako akasema huyu si shetani kabisa,
ukamjibu huyu siyo ni mwonekano tu, huyu siyo shetani, huyu ni mtu mzuri
na ana moyo mzuri,” alisema Godzilla.
Katika hatua nyingine Godzilla amezungumzia ujio wa video ya kazi hiyo ambayo amedai ndani yake kutakuwa na devil sign.
“Video yake lazima iwe ya kishetani kweli, kutakuwa na design za
devil sign zote yani, lakini huyu mtu ni mtu mzuri, kwahiyo kutakuwa na
watu wenye mapembe, yani ukiiona unaweza jua huyu ni shetani, kwahiyo
audio itatoka kesho lakini video itatoka soon na nitashoot na Nick
Dizzo.”
No comments:
Post a Comment
paulmkale