Kwanini Diamond Platnumz(@diamondplatinumz) Alilia Kwenye Video Hii?
Hakuna siri kuwa Diamond Platnumz na Yemi Alade walifanya kazi nzuri
kwenye msimu wa pili wa Coke Studio Africa. Miongoni mwa nyimbo
zilizofurahiwa zaidi ni Johny ya Yemi na..> Ukimwona ya Diamond ambazo
waliziimba pamoja.
Lakini kilichofurahisha zaidi na pengine ambacho watu wengi
hawajakigundua ni pale Diamond alikuwa akijadiliana na producer wa video
ya live performance ya ‘Ukimwona’ ambapo alikuwa akimweleza idea
mbalimbali za kuifanya vizuri zaidi.
Hata hivyo kwenye maongezi hayo Diamond alijikuta akibubujikwa na machozi kwa kukumbuka kitu cha huzuni kwake.
“This background is taking me to another world I am telling you,”
Diamond alimwambia producer huyo. “It reminds me of those days,”
anaongeza Diamond huku akiinama kuficha macho yake. “It’s a very
powerful song,” anasema producer.
“Are you okay,” producer anauliza na Diamond kusema yuko sawa ilhali akiendelea kuinama.
Swali ni kitu gani alichokikumbuka hadi kumfanya atoke machozi? Ni suala kuhusu mapenzi au maisha? Tutamuuliza tukipata nafasi!
Mashairi ya Ukimwona yalimkosha pia Yemi Alade ambaye alisema wimbo
huo una ‘content’ ya hatari kitu ambacho wasanii wengi hawaandiki.
Tazama video hiyo utaipenda.
No comments:
Post a Comment
paulmkale