Mrisho Mpoto ameungana na wasanii wengine 20 barani Afrika
kutengeneza wimbo maalum wa kuelimisha jamii kuhusiana na kupambana na
ugonjwa wa Ebola. Msanii huyo aliteuliwa na Kora kuwa balozi wa...>
Tanzania
na ugonjwa wa Ebola.
Msemaji wa Mpoto Theatre Gallery Ltd, Dominic amesema kuwa
nafasi aliyoipata Mpoto kufanya kazi na wasanii mbalimbali wa Afrika ni
njia moja wapo ya kumtangaza na kuufikisha muziki wake mbali zaidi.
“Mpoto ameshaanza kurekodi, pia hao wasanii 20 wa Afrika ambao ni
mabalozi wa kupambana na ugonjwa wa Ebola, tayari na wao wameshaanza
kurekodi. Kwahiyo ni nyimbo ya pamoja ambayo inazungumzia kupiga vita
maambukizi ya Ebola. Hii project ipo chini ya Kora, mpaka sasa hivi
maandalizi yapo vizuri na soon watanzania na waafrika kwa ujumla
wataanza kusikia project hiyo,” amesema Dominic.
No comments:
Post a Comment
paulmkale