Tarsis Masela – Chaguo Langu(Official Music Video)

RAIS wa Akudo Impact, Tarsis Masela anaendelea kuachia vitu vipya nje ya bendi yake, kama sehemu ya maandalizi ya kukamilisha albam yake binafsi
.
Baada ya kuachia audio na video ya wimbo wake mkali “Tabia Mbaya” alomshirikisha Mzee Yussuf, Tarsis Masela sasa amekuja na kitu kipya kinachokwenda kwa jina la “Chaguo Langu“. Katika kuonyesha kuwa amepania kushuka na vitu vilivyojaa viwango, Tarsis Masela hivi karibuni alikwenda jijini Nairobi nchini Kenya kuandaa video ya wimbo huo kupitia kampuni ya E-World Productions Films chini ya mtayarishaji wake Papa Vir ambaye pia ni mtangazaji.
Tarsis ameiambia DJChokaMusic kuwa amekwenda Kenya kufuata viwango na kuleta utofauti. “Papa Vir ni mtayarishaji wa kimataifa, nina imani video hii italeta mapinduzi kwenye muziki wa dansi,” alisema Tarsis Masela.

No comments:

Post a Comment

paulmkale