Video mbili za ‘Akadumba’ zimemkamua shilingi milioni 36 Nay wa Mitego
Nay wa Mitego amekata mpunga mrefu kushoot video mbili tofauti za ngoma yake ‘Akadumba’
Nay amesema kuwa, shilingi milioni 36 zimetumika kukamilisha mzigo huo.
“Kiukweli kabisa imenigharimu pesa nyingi sana ambayo sikufikiria
kama inaweza ikanigharimu kiasi hicho,” amesema Nay. “Nilikuwa natafuta
kitu kizuri na kuwaonyesha watu nini kinatufanya tutoke nje. Kwahiyo
video moja nimefanyia nchini Kenya na Kelvin Bosco na moja
nilimsafirisha akaja hapa nyumbani Tanzania, zote kafanya yeye. Kwahiyo
zote zipo tayari. Zimegharimu zaidi ya milioni 36. Kwahiyo mpaka sasa
hivi ninaweza nikasema zitatoka kabla mwaka huu haujaisha. Moja itatoka
Alhamis ijayo ambayo nimefanyia nyumbani na hii nyingine itatoka mwaka
huu huu.”
No comments:
Post a Comment
paulmkale