Kaa Tayari;Mrisho Mpoto kuachia wimbo mpya ‘Njoo Uichukue’

Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto anatarajia kuachia wimbo mpya uitwao ‘Njoo Uichukue’Mpoto, amesema wimbo huo utawafungua watu macho na kuwapa mwanga kuvifuata vitu vizuri wanavyovihitaji.

“Mpaka sasa naendelea kuwepo kwenye muziki ni kwa sababu ya mashabiki wangu. Wasikilizaji wangu au mashabiki wangu wana uwezo mkubwa wa kutafakari nyimbo zangu mpaka wakati mwingine wananishinda mimi mwenyewe, ndio maana wakati mwingine wananipa kazi ya kukaa mwaka mzima kuwafikiria nitawapa kitu gani,” amesema Mpoto.

“Kwahiyo mimi naamini huu wimbo utawafungua watu na kuwapeleka kwenye vitu wanavyovihitaji. Wimbo utatoka Jumatatu ijayo na umetengenezwa ndani ya studio yangu.”

No comments:

Post a Comment

paulmkale