Mo Music aingia kwenye biashara yake ya Dagaa na Senene

Basi nenda hit maker "Mo Music" baada ya ku-release double singles mwishoni mwa mwaka jana, sasa hivi ame introduce biashara yake ya kuuza SENENE na DAGAA wa Mwanza ili kusapoti maisha yake ya upande mwingine."Hii biashara haina mda mrefu na si senene peke yake, kuna senene kuna dagaa ambazo zipo kwenye package mbali mbali inategemea na mteja wangu anahitaji nini...kwa Dar ndio inakuwa supplied sana, mkoa ambao una oda nyingi ni Dar, mwanza na morogoro sehem zingine zingine hawajaamka sana lakini mikoa hiyo ndio wanaochukua sana bidhaa hizo kwa mwaka jana..... Watu wanasahau kuwa biashara ndogo ndogo na ambazo zinasahaulika ndio ambazo kidogo zinaweza zikakusukuma katika maisha..........." amesema Mo Music
Wasanii wengine wenye biashara zao zinazofahamika nje ya muziki ni Jafarai  na Jafary’s Car Wash, Jokate na mtiririko wa bidhaa zake za ndala na nywele, Man Dojo na Domokaya wana duka la nguo na viatu, Masanja Mkandamizaji ana kampuni yake ya ulinzi, Izzo Business ana duka na Stationery, list inaendelea

No comments:

Post a Comment

paulmkale