Kauli Ya Young Dee Yakera Bloggers Na Mkito Iongeze Malipo yake Kwa Bloggers wote Kama Mdau Wa Muziki Hii Inakuhusu

Ifike kipindi Wasanii wa Muziki wasijisaulishe bali wakumbuke wapi walianzia na mpaka kufika leo ni support gani wamepewa na Blogs mpaka kufika hapa.
Leo nimesoma habari kutoka Bongo5 yenye kichwa cha habari hiki "Exclusive: Young Deeatoa ujumbe muhimu kwa blogs za burudani Tanzania" Huu ni mtazamo wake kwenye kazi yake lakini ni vema angefikiri kwanza kabla ya kuwa mbinafsi.

Sipingi swala la Msanii kuuza nyimbo zake MKITO hapana cos hiyo ni haki yake, lakini kabla msanii hajaanza kuangusha lawana kwanza angejiuliza tatizo lipo wapi? naamini wao ndio wangekuwa watu wa kwanza kuwatetea Bloggers ili nao waboreshewe malipo yao kama vile ambavyo wao wanapokea hizo Millioni zao. Badala yake unakuta Msanii anajitoa fahamu na kuanza kuongea kwamba hataki nyimbo zake ziwekwe sehemu nyengine zaidi ya MKITO sasa mbona wakati tunasambaza na kuwekeza nguvu kwenye promo ya nyimbo zenu bila hata kutoa Senti 5 hamkuwa na kauli mbovu hivi?!
Naheshimu sana kazi ya Msanii maana ndio kitu kinachompa kula, lakini ifike wakati Wasanii nao waheshimu Blog na mitandao mingine yote ambayo ina support kazi zao kwa namna moja ama nyengine.

Wiki chache zilizopita aliyekuwa Editor wa Blog hii alitumiwa wimbo wa Gosby - Noma ili kupandishwa kwenye Blog naye alichukua wimbo huo na kuupandisha lakini hakutumi link ya Mkito, baada ya masaa kadhaa nikapokea simu kwa mtu ambae ana uhusiano na Gosby na kuhoji kwanini haijatumika link ya Mkito? Nilijaribu kumuelewesha kwanza Editor hakuwa anaelewa chochote kuhusu Mkito pili Nilijaribu kumuelewesha kuhusu mfumo mzima wa malipo na yeye akanijibu hakujua hilo nikamwambia ni vema wasanii nao waangalie upande wa Blogs ambazo ndio source kubwa ya kuingiza hizo pesa nao at least walipwe vizuri lakini hiyo story iliishia hapo na sijui kama aliwekea maanani jambo hilo.

Pia Mkito nao wabadili mfumo wao maana sidhani kama unamfaidisha Msambazaji (Blog) bali unazidi kumuumiza, unakuta malipo yanayoenda kwa Blog inayopost wimbo ni Tshs. 3 tu kwa download moja sasa kwa hesabu ya haraka haraka tu zidisha hiyo Tshs 3 kwa Download 1,000 unapata 3,000 ambazo kwa Mkito kuzipata ni ngumu sana kutokana na mfumo wao wa ku download wimbo. Tunaambiwa kwamba tunalipwa kwa asilimia bila kuoneshwa mkataba wa malipo ambayo kampuni inayotangaza imelipa kiasi kadhaa hivyo kutokana na mgawanyo wa kiasi hicho blog itapata hiki, Msanii hiki na wao wenyewe watabaki na asilimia zao, lakini tunalazimishwa kuamini hata kama sio kweli.

Ifike muda Bloggers tuthaminiwe kwa kile ambacho tunafanya, na vitu kama hivi ndio vinasababisha ugumu kwa wasanii chipukizi kutoka au ngoma zao kufika sehemu nzuri, kama kungekuwa na mfumo ambao unafaidisha pande zote naamini wasanii chipukizi wengi wangefurahi maana wangesikika kirahisi bila changamoto yoyote ile.

Najua wengi wanatamani kuongea mengi kuhusu hii issue na kutoa madukuduku yao bali nidhamu ya woga inachangia, Najua baada ya post hii wapo ambao watachukia na kuchukua maamuzi wanayoyajua wao pia wapo ambao watanielewa na kujua tatizo lipo wapi.
Asante.

No comments:

Post a Comment

paulmkale