Kundi
la Muziki wa Kizazi kipya Yamoto Band wanatarajia kuanza safari yao ya
kwenda UK kufanya Show tarehe 17 mwezi huu na show itapigwa Tarehe 21
ndani ya Royal Regency.
Mkurugezi wa
Kundi hilo Mkubwa Fella kwanza alianza kwa kutoa shukran zake kwa
Mwenyezi Mungu, Mashabiki, Wadu na vyombo vyote vya habari kwa kuweza
kutoa sapoti kwa vijana hao tangu walipo toa Kazi yao ya kwanza kabisa
mpaka kufikia Leo wamepata mualiko mkubwa kabisa wa kwenda kufanya show
UK, na kwa upande wa Msemaji mkuu na Kiongozi wa Band Aslay Isihaka
amesema kuwa wanafuraha sana kwa kupata mualiko huo lakini pia
wanashukuru kwa mungu, mashabiki na wale wote wanaonyesha sapoti katika
muziki wao. Aslay amesema kuwa watakwenda kufanya Kazi nzuri huko ili
kuleta sifa ya muziki wa hapa nyumbani na hata heshima ya Taifa kwa
ujumla.Kwa upande mwingine Vijana hao Wametoa shukrani zao kwa Viongozi
wao Mkubwa Fella, Bab Tale, Chambuso, Mh Temba na Shirko kwa usimamizi
Mzuri wa Kazi hizo.
No comments:
Post a Comment
paulmkale