Mwanamuziki Hemed PHD Katika Skendo ya Utapeli..Achukuliwa RB Asakwa Usiku na Mchana
Kha! RB namba KTN|RB/11213/2014 –UTAPELI inamsaka msanii wa muziki na
sinema za Kibongo, Hemed Suleiman ‘PHD’ tangu mwaka jana, akidaiwa
‘kuchikichia’ nguo za shilingi laki saba, mali ya aliyekuwa Mtangazaji
wa EATV, Nasra Dattani ‘Lady Naa’ ambaye alimkabidhi begi lake la nguo
baada ya kumaliza kurekodi filamu iitwayo Catherine.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Lady Naa alisema kuwa alimvumilia Hemed
kwa muda mrefu kwani alimpa mzigo huo na kumuomba akaushushe dukani kwa
rafiki yake maeneo ya Kinondoni lakini hakufanya hivyo na alipokuwa
akimkumbusha alikuwa akimwambia kuwa atampelekea.
“Kila nikikutana naye nilikuwa namuomba anirudishie anasema nifanye
lolote na kinachonishangaza amezipeleka wapi maana mle kulikuwa na nguo
za kike ambazo nilizitoa Uingereza,” alisema Lady Naa.
Alidai kwamba baada ya kumzungusha kwa muda mrefu ndipo alipoamua
kumfungulia kesi kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama, Dar ambapo
hadi leo anasakwa. Baada ya habari hizo kulifikia gazeti hili,
mwanahabari wetu alimwendea hewani Hemed lakini namba yake haikupatikana
hivyo jitihada zinaendelea. -
No comments:
Post a Comment
paulmkale