KWA mara ya kwanza baada ya miaka mingi, ukumbi wa
Mango Garden, ulioko Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kupitisha wikiendi
bila burudani yoyote, leo usiku ‘utawaka moto’ wakati Yamoto Band na
Mashauzi Classic zitakapotoa shoo kabambe hapo.
Ni onyesho ambalo limeteka hisia za mashabiki wa muziki kutokana na
ukweli kuwa vikundi hivyo viwili havijawahi kukutana katika katika
onyesho la pamoja, ukiondoa yale matamasha yanayoshirikisha wasanii
wengi.
Kesho, Ijumaa, Malaika Band ambao hupiga hapohapo Mango Garden, kila Ijumaa, watakuwa Arusha mjini wakitoa burudani.Mwimbaji na Kiongozi wa Kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’.
Vilevile, Twanga Pepeta ambao hupiga Mango Garden kila Jumamosi,
wasanii hao Jumamosi hii watakuwa Wenge Garden Ukonga. Bendi ya FM
Academia ambayo huibuka Mango Garden na kufukia viraka vya bendi
zilizopata dharura ya kuhama ukumbi, Ijumaa hii itakuwa Polisi
Kilwa Road wakati Jumamosi itakuwa Leaders Club katika tamasha la Nyama Choma.
No comments:
Post a Comment
paulmkale