Collabo ya Joh Makini na AKA, Video Kufanyika South Afrika.

Baada ya kufanya Vizuri na Video ya "Nusu nusu" Joh Makini anatarajia kufanya Video ya Nyimbo aliyomshirikisha Rapper kutoka South Afrika maarufu kama AKA.
"Kusema kweli nimeuona mwanga mkubwa sana wa muziki wa Hip Hop ya Tanzania kimataifa tofauti hata nilivyokuwa nimetarajia, jinsi ambavyo watu wanarespond hii ngoma (Nusu Nusu) nje ya nchi, ni kitu ambacho yani unajua kuna step ukipiga unakuwa kama mteja, ili uweze ku-maintain hiyo step pale inabidi upambane, Sasa inabidi niende kufanya video ya ngoma ambayo nimefanya na AKA anytime soon, tulifanya hapa hapa Bongo alipokuja jamaa kwenye show ya Zari All-White Party. Nafikiri ndio ngoma ambayo naenda kushoot lakini ni mapema kusema ndio itafata kwenye audio, naweza nikatoa ngoma nyingine tofauti kwenye audio halafu hiyo niliyofanya na AKA natarajia kuiachia video kwanza." alisema Joh Makini.

No comments:

Post a Comment

paulmkale