Mwaka huu Tanzania inawakilishwa na wasanii wawili kwenye tuzo za MTV Africa Music Awards KWAZULU-NATAL 2015 (MAMA), ambao ni Diamond Platnumz pamoja na Vanessa Mdee.
Ili Diamond na Vanessa waweze kushinda, nguvu kubwa inahitajika kutoka
kwa mashabiki kwa kupiga kura kwa wingi sababu ushindi wa mabalozi hawa
wa burudani ni ushindi kwa taifa zima la Tanzania.
Diamond anawania vipengele vitatu ambavyo ni Best Male, Best Collaboration na Best Live.
Upande wa Vanessa anawania kipengele kimoja cha Best Female.
Njia ya kupiga kura ni moja, ingia kwenye website ya http://mama.mtv.com/voting/ na ufate maelekezo rahisi ya jinsi ya kupiga kura.
Support muziki wa nyumbani ili uweze kufika mbali kimataifa.
No comments:
Post a Comment
paulmkale