Mfahamu zaidi hapa Director Meji Anaeshoot video mpya ya Alikiba.

Msanii Alikiba alikuwa nchini Afrika Kusini akifanya video yake mpya anayotarajia kuitoa hivi karibuni na director, Meji Alabi mwenye makazi yake katika mji wa London huko England...Kwa siku kadhaa Alikiba amekuwa akipost picha na Director Meji ambae ameishi nchini Marekani kwa muda mrefu na kuwa na uzoefu wa kushoot video za kampuni kubwa kama Beats by Dre na video tofauti za wasanii pamoja na filamu. Je wajua Director Meji ndio alifanya video ya Beats By Dre x Berlin x Axwell

Mjue kwa Undani Director Meji ...


Kupitia Tovuti ya Director Meji iitwayo  'http://mejialabi.com  

ameandika wasifu wake na pia kuorodhesha kazi ambazo

ameshawahi kuzifanya ikiwemo Tangazo la Beats by Dre x Berlin x Axwell.

Video hio ya kampuni ya Beats ilifanyika huko Berlin mwaka 2013 katika sherehe ya 

kuzindua Studio mpya za beats. Sherehe hio ilihudhuriwa na dj's tofauti 

pamoja na Rapa maarufu nchini Uingereza Tinie Tempah na Giggs

Meji  amekuzwa nchini Marekani ila kwasasa makazi yake yapo katika mji wa London huko England. 

Meji pia amefanya kazi za aina tofuati kuanzia za muziki mpaka documentaries. Kazi yake ya hivi karibuni aliofanya Meji ni video ya Asa - Eyo (Click kuangalia video hio) pia unaweza kuangalia video ya Beats-By-Dre-x-Berlin-x-Axwell iliofanywa na Meji.

katika Wasifu wake Meji aliandika anapenda kutengeneza Filamu pia.


No comments:

Post a Comment

paulmkale