Cheza Kwa Madoido‘ ndio hit nyingine mtaani kwa sasa, kazi nzuri kutoka kwa Yamoto Band.. Hongera nyingi ziende kwao kwa ushindi wa Tuzo moja ya #KTMA2015 category ya Kundi Bora la Muziki #BongoFleva.
Leo June 15 2015 Timu nzima ya Yamoto Band wamekwea pipa kwenda South Africa kwa ajili ya kushoot video yao mpya ya hit hiyohiyo ya Cheza Kwa Madoido.
Mkubwa Fella ambae ndio Meneja wa Kundi hilo amesema kwanza anamshukuru Diamond
kwa kuwapiga tafu madogo ili nao watoboe kama ilivyokuwa kwake kwani
mipango yote ameifanikisha yeye na leo usiku wanaanza mchakato mzima
kuifanya video hiyo.
Kazi ya Video imekabidhiwa kwa Director Godfather kwa gharama ya kama Dola Milioni mbili hivi.. Hizo zimetolewa na Diamond Platnumz pia !!
No comments:
Post a Comment
paulmkale