Collabo
ya hivi karibuni aliyofanya Diamond Platnumz ni alioshirikishwa na
Kcee, Kumekuwa na maoni tofauti ya wadau wa Muziki ambao wameonesha moja
kwa moja kuwa hawaukubali wimbo huu.
Haya ni Baadhi ya maoni ya watu mbalimbali katika mtandao wa Jamii Forum..
"Wakuu
nimesikiliza tena huu wimbo mpya wa KCE feat Diamond, ni wazi kabisa
huenda Dai hakujiandaa au alivamia tu collabo la watu.
Ukisikiliza kwa umakini utaona kuwa, Sauti ya Dai imebanwa na
haisikiki vizuri kabisa, sijui huu ndio ubanajai pua mpya au ndio
unaijeria umezidi kwa huyu mzalendo wetu?
My take: Kwa hali hii watanzania tuna haki ya kumpa kura Davido" Hayo ni maoni ya SHARDCOLE.
"Hilo
la sauti limeshakuwa tatizo kwake sasa aliwahi haribu hata nyimbo ya
Waje Coco, Pia mimi tokea aharibu kwenye ule wimbo wa Prof J siumizi
tena kichwa.
Huwezi kulinganisha wimbo wowote alioshiriki diamond na Kiboko Yangu ambapo King aliua vibaya sana.
Hakika Ali Kiba is gifted!" haya ni maoni ya Nifah.
No comments:
Post a Comment
paulmkale