Diamond Platnumz Ametajwa Tena Kuwania Tuzo Hizi Za Nchini Marekani.

Wakati Watu wakiwa na hamu ya kupata matokeo ya tuzo za MTV ambazo Diamond ni mmoja wa washiriki  katika Tuzo hizo  Diamond anazidi Kupata nafasi  zaidi baada ya kutajwa katika tuzo za African Entertainment Awards za Nchini Marekani.
 Diamond amekuwa nominated katika vipengele  viwili ambavyo ni Hottest Male(Msanii bora wa kiume) na Single Of The Year(wimbo bora wa Mwaka-Ntampata Wapi).

Diamond amepost katika mtandao wa Instagram akitoa shukran zake...ameandika "Naomba niwashkuru wadau na Mashabiki zangu wote kwa support kubwa mnayozidi kunipa... Niwashkuru wote mlokuwa Mkihamasisha na kupiga kura katika tunzo za #Mtvmama2015 Hakika ni upendo Mkubwa..kijana wenu now nimetua South Africa tayari kwajili ya Kujiandaa kwa show nk... ila pia wakati nimetua nimekutana na Habari nyingine nzuri...kuwa Nimechaguliwa kwenye Tunzo za Marekani ziitwazo @AfricanEntertainmentAwards Kama Msanii Bora wa Kiume Africa na Nyimbo bora ya Africa #NtaMpataWapi Hii ndio Account yao @AfricanEntertainmentAwards Ntawajuza namna ya Kupiga kura Soon".

No comments:

Post a Comment

paulmkale