Wiki iliyopita Diamond Platnumz alizusha mjadala mkubwa sana kuhusu
kauli aliyoitoa katika kipindi cha Papaso kinachoongozwa na Djaro
Arungu, Diamond Platnumz alisema kuwa akiamua kuwabania wasanii wa Bongo
ana uwezo huu kwa sababu yeye anahusika kupitisha nyimbo za bongo
zinapopelekwa katika kituo cha Television cha MTV.
Babu Tale katika kipindi cha XXL amesema “Ingekuwa kweli
nyimbo ya Harmonize ambaye ndio msanii wa Diamond, ingekuwa Exclusive
MTV au ingekuwa inapigwa kila siku kwasababu ndio biashara yake, si
ndio, hilo sio neno la kweli, yule aliyetoa hiyo habari amechukua kichwa
cha habari na kukinya habari kwa watu wengine…..Diamond alihojiwa,
alikuwainterview kwenye.. moja ya swali aliloulizwa wasanii gani ambao
umewasaidia, na je, unasupport mziki wa nyumbani kwenda nje? yeye
akajibu mbona mimi nasaidia watu wengi na kuna kipindi huwa napigiwa
simu mtu anauliza labda unamjua fulani mzuri? kuna vipindi, media za nje
huwa zinanipigia unamjua fulani mzuri? me nawaambia mzuri kwasababu ya
kutengeneza mazingira watu wote tutoke tutangaze mziki wetu nje,
alieandika kile kichwa cha habari akasema kwamba Diamond ndiye anayeamua
myimbo fulani kwenda sehemu fulani kitu ambacho siyo cha kweli, kama
Diamond angekuwa anaamuahivyo maana yake hayo maamuzi anafanya na
menejimenti basi nyimbo zote za sijuhi TMK, za TipTop, za mkubwa na
wanawe za watu wote wa karibu na Diamond wote ndio zingekuwa zinapigwa
sana kuliko hata wengine.“
No comments:
Post a Comment
paulmkale