Baraza
la Mitihani la Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya mitihani ya
kujipima ya darasa la nne huku matokeo hayo yakionyesha wanafunzi wengi
wamefeli katika somo la Kiingereza kwa asilimia 65.67 katika mitihani
hiyo iliyofanyika mwishoni 2015.
Akitangaza
matokeo hayo leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo
Dkt. Charles Msonde amesema juhudi za makusudi zinahitajika katika
kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzia ili kuboresha kiwango
cha ufaulu.
Jumla
ya wanafunzi 869,057 kati ya wanafunzi 977,886 sawa na asilimia 88.87
waliofanya upimaji wamepata alama katika madaraja ya A,B,C,na D.
Wanafunzi 108,829 sawa na asilimia11.13 wamepata alama za ufaulu
usioridhisha.
==>Bofya Hapa Kuyaona Matokeo
No comments:
Post a Comment
paulmkale