Na Veronica Simba – Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa amefanya
ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na
Chuo cha Madini Dodoma (MRI).
Ziara
hiyo iliyofanyika jana Januari 13, 2016 mjini Dodoma, ziliko Taasisi
hizo, ililenga kujitambulisha kwa viongozi na watumishi pamoja na
kujionea kazi na huduma mbalimbali wanazotoa kwa wananchi.
Katibu
Mkuu alikutana na viongozi wa GST na wa Chuo cha Madini ambapo alipokea
taarifa ya utendaji, kisha akakutana na wafanyakazi wote wa Taasisi
hizo na kuzungumza nao kuhusu majukumu yao na changamoto walizonazo
kiutendaji.
Baada
ya kukutana na Wafanyakazi, Katibu Mkuu Ntalikwa alitembelea majengo
mbalimbali ya Wakala kujionea kazi zinazofanyika ambapo ni pamoja na
Maabara mpya ya kisasa ya Uhandisi wa Kijiolojia, Chumba chenye mitambo
na mashine za kisasa zinazohifadhi data mbalimbali, chumba maalum
kinachohifadhi nyaraka na machapisho mbalimbali pamoja na Maabara ya
kuchenjua Madini (Mineral processing Laboratory).
Ziara
ya Katibu Mkuu Ntalikwa katika Ofisi za GST na MRI ni mwanzo wa ziara
anayofanya kutembelea Mashirika na Taasisi mbalimbali zilizo chini ya
Wizara ili kujitambulisha na kujionea kazi na huduma wanazotoa. Profesa
Ntalikwa ataendelea na ziara mjini Dodoma kwa kutembelea Ofisi za
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Ofisi za Shirika la Ugavi wa
Umeme Tanzania (Tanesco).
Mtumishi
katika Maabara ya Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Kamana Camilius
(mwenye Koti la Bluu) akimweleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini (wa pili kutoka Kulia) namna Maabara hiyo inavyofanya kazi.
Wengine pichani ni Viongozi wa GST.
Mtumishi
katika Maabara mpya ya kisasa ya Uhandisi wa Kijiolojia inayomilikiwa
na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Godson Kamihanda (wa pili kutoka
Kushoto) akimweleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
(katikati) namna Maabara hiyo inavyofanya kazi. Wengine pichani ni
Viongozi wa GST.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (mbele)
akikagua Jengo jipya la Ofisi ya Madini – Dodoma. Pamoja naye pichani ni
Viongozi wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST). Jengo hilo lipo jirani
na Ofisi za GST.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa akisaini
Kitabu cha Wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma (MRI)
alipotembelea Chuoni hapo hivi karibuni.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa
akisalimiana na Watumishi wa Chuo cha Madini Dodoma (MRI) alipowasili
ofisini kwao kuwatembelea na kuzungumza nao hivi karibuni. Kulia kwa
Katibu Mkuu ni Mkuu wa Chuo, Ofolo Ngowi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (mwenye
suti ya Bluu – katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na
Wafanayakazi wa Chuo cha Madini Dodoma, alipowatembelea na kuzungumza
nao hivi karibuni. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Profesa
Abdulkarim Mruma na kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo, Ofolo Ngowi.
Mkuu
wa Maabara ya Madini inayomilikiwa na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST),
Heri Issa (wa pili kutoka Kulia) akimweleza Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Profesa James Ntalikwa (katikati) namna Maabara hiyo
inavyofanya kazi. Wengine pichani ni viongozi na watumishi wa GST.
No comments:
Post a Comment
paulmkale