Baada ya Diamond kuweka wazi kuwa kituo cha runinga cha kimataifa, MTV
Base huwa wanampigia kuidhinisha video yoyote inayotumwa kwenye kituo
hicho kutoka Tanzania ili azitolee maoni kama zipitishwe ama laa, kauli
hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti na wadau wakiwemo wasanii wenyewe.
Miongoni mwa wasanii waliozungumza kuhusu kauli hiyo ni pamoja na
Alikiba, ambaye itakumbukwa kuwa video zake hazioneshwi na kituo hicho,
kitu kinacholeta sintofahamu pia kutokana na tofauti zake na Diamond.
“Nitawaambia ukweli ambao unawahusu, kama ni kweli watakuwa wanakosea
(MTV), haikai sawa na sidhani kama ni kweli,” alisema Alikiba kupitia
255 ya XXL alipoulizwa maoni yake kuhusu swala hilo.
“Yaani haikai sawa na sidhani kama ni kweli, kwasababu watakuwa
hawako fair, ndio hivyo hawako fair, hajabeba talent ya kila mtu
(Diamond), kila mtu ana kipaji chake na kila mtu ana haki ya kuonesha
kipaji chake kazi yake. Unajua kila mtu anafanya biashara ya muziki
saizi, sio mtu anafanya masihara unapoona mtu anafanya video yake
anagharamikia unajua haipendezi, kwahiyo sidhani kama ni kweli.” Alisema
Alikiba.
Kauli ya Diamond aliitoa alipokuwa akieleza jinsi wasanii
wanavyomtupia lawama kuwa anawanyima connections za kung’ara kimataifa,
“mimi nashangaa sana kusikia hayo maneno, wanasema hivyo wakati mimi
najitahidi kuwasaidia wenzangu tutoboe wote, kila kolabo ya msanii wa
nyumbani na msanii wa Nigeria inayofanywa mi ndio huwa nasababisha”
alisema Diamond.
“Nikiamua kubana mbona naweza tu, kwasababu vituo vingi vya nje
vinanisikiliza kwa mfano tu MTV wenyewe wakipokea video ya msanii yeyote
kutoka hapa (Tanzania) wananipigia wananiuliza kwanza huyu vipi?
Tuicheze ngoma yake au? Mimi huwa nasema anafanya vizuri huku, basi
inapita wanaicheza nikiamua kubana si naweza tu.” Alisema Diamond.
No comments:
Post a Comment
paulmkale