Amiri
Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli akisalimiana na wananchi wa Arusha Mjini wakati akipita
kuelekea Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli ambako pamoja na
mambo mengine kesho tarehe 23 Januari, anatarajiwa kutunuku Kamisheni
kwa Maafisa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kundi la
57/15.
Amiri
Jeshi Mkuu,Rais Dkt Magufuli akiwasikiliza wananchi kwa makini
alipopita maeneno ya Sanawali kuwasalimia wakati akielekea Wilayani
Monduli.
Baadhi
ya Wananchi wa Maeneo ya Sanawali wakishangilia ujio wa Rais John Pombe
Joseph Magufuli,alipokuwa akielekea Wilayani Monduli mapema leo
asubuhi.
Rais
Magufuli akiwa amevalia sare za kijeshi amesimamishwa na kuwasalimu
wananchi katika maeneo ya SANAWALI, TEKNIKO, NGARENALO, MBAUDA, MAJENGO
na KISONGO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na wananchi wa Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha waliojitokeza
kumsalimia wakati akielekea Monduli kwa ajili ya kufunga zoezi la Onesha uwezo
Medani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mbauda Mkoani Arusha hawaonekani
pichani wakati akielekea Monduli kwa ajili ya kufunga zoezi la Onesha uwezo
Medani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akisoma bango alilokabidhiwa na mwananchi mmoja
katika eneo la Kona ya Nairobi Mkoani Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwahutubia wananchi wa Arusha katika eneo karibu na chuo cha Arusha Tech.
Wananchi hao walifunga barabara ili wapate nafasi ya kumuona Mheshimiwa Rais
Dkt. Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mianzini Mkoani Arusha.
Umati mkubwa uliojitokeza katika eneo la Mianzini Mkoani
Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General
Davis Mwamunyange wakati waufungaji wa zoezi la Onesha Uwezo Medani
lililofanyika Monduli nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akijadiliana jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis
Mwamunyange wakati akielekea kupewa maelezo ya zoezi zima la Onesha Uwezo
Medan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa jeshi katika tukio hilo la
Ufungaji.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akielekea kwenye uwanja wa maonesho akiwa pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
Nchini General Davis Mwamunyange.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni
Sefue, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Ntibenda, Mkuu wa Majeshi
Jenerali Davis Mwamunyange na Maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi mara
baada ya kufunga zoezi la Onesha Uwezo Medani Monduli Mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli katikati akishuhudia matukio ya zoezi la Onesha Uwezo Medani
Monduli Mkoani Arusha.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli ameonya kuwa wilaya ama Mkoa wowote ambao utakumbwa na
njaa, itakua ni kipimo tosha cha kuonesha kuwa Mkuu wa Mkoa ama Mkuu wa
wilaya husika hafai kuendelea na wadhifa huo.
Rais
Magufuli ametoa onyo hilo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti
aliposimamishwa na wananchi wa Arusha Mjini akiwa njiani kuelekea
Monduli ambako amefunga "Zoezi Onesha Uwezo Medani" lililoandaliwa na kutekelezwa na kamandi ya Jeshi la nchi kavu ambalo ni sehemu ya jeshi la wananchi wa Tanzania.
Amesema
kwa kuwa mvua zinaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi,
Viongozi wa Wilaya na Mikoa wana wajibu wa kuwahamasisha wananchi
kuzalisha mazao ya chakula ili wasikumbwe na njaa.
Rais
Magufuli ameendelea kuwasihi wananchi wa Arusha Mjini kuwa uchaguzi
umekwisha na kwamba kilichobaki sasa ni kazi huku akiwahimiza kufanya
kazi za uzalishaji mali ikiwemo kilimo.
"Naomba
ndugu zangu mniombee, na ninapenda kuwahakikishia kuwa sitawaangusha.
Yote niliyoahidi nitayatekeleza bila kubagua nawaombeni mnipe muda na
muwe wavumilivu" alisisitiza Rais Magufuli.
Amerejea
kauli zake alizozitoa jana alipoingia mkoani Arusha kuwa atendelea
kuwashughulikia wezi, mafisadi na watendaji wote wa serikali ambao
wamekua wakijineemesha kwa kufuja mali ya umma kupitia kampeni yake ya
"Kutumbua Majipu" na amewaomba watanzania wote waendelee kumuombea ili
atumbue majipu yote hadi yaishe.
Rais
Magufuli amelazimika kuzungumza na wananchi wa Arusha Mjini waliokuwa
wamekusanyika kwa maelfu kando kando mwa barabara na hivyo kujikuta
akisimamishwa na wananchi wa Sanawali, Tekniko, Ngarenaro, Kona Ya Nairobi, Mbauda, Majengo Na Kisongo.
Akiwa
katika eneo la Ngarenaro wananchi wamelalamikia vitendo vya rushwa
vilivyokithiri katika mahakama ya mwanzo ya Maromboso na pia katika eneo
la Kona ya Nairobi wananchi wamelalamikia kero za kelele na uchafu wa
kiwanda kilichojengwa kandokando mwa barabara ambapo Rais Magufuli
ameahidi kufanyia kazi kero hizo.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Arusha.
22 Januari, 2016.
No comments:
Post a Comment
paulmkale